TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday, 8 May 2012

NASARI AGWAYA KUKAMATWA, AJISALIMISHA POLISI



MBUNGE wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari (Pichani) ametii amri ya polisi baada ya kuibuka na kujisalimisha leo makao makuu ya polisi mkoa wa Arusha kufuatia agizo la jeshi hilo lililotolewa jana na mkuu wa kitengo cha ufuatiliaji na tathimini Naibu kamishna wa polisi Issaya Mngulu la kumtaka mbunge huyo kujisalimisha kutokana na maneno yake ya uchochezi.
Nassari alijisalimisha kituoni hapo majira ya saa tano asubuhi na kasha kulazimika kuondoka kituoni hapo baada ya kuwakosa kaimu kamanda wa polisi mkoani Arusha Akili Mpwapwa pamoja na Naibu kamishna Issaya Mngulu waliokua wakihudhuria kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.
Mara baada ya kuondoka kituoni hapo Nassari alirejea tena kituoni hapo baada ya nusu saa akiwa na wakili wake Albart Msando ambapo alipokelewa na kaimu kamanda na kasha kukutanishwa na Issaya Mngulu na viongozi wengine wa polisi mkoa tayari kwa mahojiano.
Kwa upande wake Nassari alipoulizwa kwanini alikaidi kutii amri ya polisi iliyomtaka kufika kituoni kwa mahojiano alisema hakupata taarifa hizo bali taarifa alizozipata za polisi ni kutoka kwa aliyekua kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Thobias Andengenye kupitia kwa ofisa mmoja wa polisi kuwa alimuhitaji kufika kituoni hapo kwaajili ya kuagana baada ya kamanda huyo kupata uhamisho kwenda jijini Dar es salaa kikazi.
Mahojiano hayo ambayo mpaka tunakwenda mitamboni yalikua yakiendelea kwa zaidi ya saa sita mpaka saa 11 jioni Nassari alikua akiendelea kuhojiwa kuhusiana na tuhuma hizo zinazomkabili ikiwemo za kutoa kauli za uchochezi katika mkutano wa hadhara uliofanyika siku ya jumamosi iliyopita katika uwanja wa NMC Unga Ltd mjini Arusha.
Hata hivyo muda wote akiwa anaendelea na mahojiano aliyekua mbunge wa Arusha mjini Godbles Leman a wafuasi wengine wa Chadema walionekana nje ya viwanja vya makao hayo makuu ya polisi ambapo hata hivyo baada ya muda waliondoka pasipokujilikana walikoelekea.
Kwa mujibu wa Kamishna Mngulu hapo jana a.lipozungumza na vyombo vya habari alidai kuwa Nassari alisikika akitamka maneno hayo ya uchochezi kwa kulipa jeshi la polisi siku tatu kuwapata waliosababisha kifo cha aliyekua mwenyekiti wa Chadema kata ya Usa River wilayani Arumeru Msafiri Mbwambo la si hivyo Rais Kikwete pamoja na Waziri Mkuu Pinda wasikanyage Arusha.
 Pia alisema mara baada ya kauli hiyo Nassari alijitangaza kuwa yeye ndiye Rais wa Arusha huku akimtangaza aliyekua mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema kuwa waziri mkuu.
Mngulu alisema kauli nyingine ni ile ya kutangaza kuiunganisha mikoa ya kanda ya kaskazini na ile ya kanda ya ziwa kuwa nchi inayojitegemea yaani kujitangazia jamuhuri yake binafsi kama ilivyotokea Sudan Kusini.
Pia alisema kauli nyingine ni ile iliyomuhusu motto wa Rais Kikwete Ridhiwana Kikwete kwamba ana marafiki zake wa kike na kazi yake ni kuwatambulisha kwa baba yake ili awateue katika nafasi mbalimbali za uongozi na kwamba Rais Kikwete anateua viongozi kwa kushauriwa na Ridhiwan.
 Kauli nyingine ni ile ya kutafuta vijana wapatao 500 ili kufanya maandamano hadi ikulu ya magogoni jijini Dar es salaam kutokana na nchi hii kutafunwa na wajanja huku Rais Kikwete akiangalia tuu.
Mbali na ,mbunge huyo kuhojiwa viongozi wengine watatu wakiwemo na wanachama wa chama hicho walihojiwa hapo jana kwa tuhuma hizohizo akiwemo mwenyekiti wa baraza la vijana wa Chadema taifa John Heche,aliyekua mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Arusha Ally Bananga aliyehamia Chadema hivi karibuni na aliyekua diwani wa kata ya Sombetini CCM Mawazo Alphonce aliyehamia Chadema hivi karibuni.
Hata kamishna Mngulu alisema mara baada ya mahojiano hayo jeshi lake litaandaa jalada la kesi la kuliwasilisha kwa mwanasheria mkuu wa serikali ili kuipitia na kuona iwapo kuna kesi ya kujibu au laa na kama ipo watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao.

No comments:

Post a Comment