Ma-DC 51 wafyekwa
*Ateua wapya 70,wabunge nao wamo
*Wengine 63 waendelea na mikoba
*Waandishi wa habari nao wapeta
*Wamo waliopikwa na B/Times, RTD
Na Peter Mwenda
RAIS Jakaya Kikwete amewateua wakuu wa wilaya 133 kati yao wa zamani 63 na wapya 70 wakiwemo waandishi saba wa habari wa vyombo mbalimbali nchini.
Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda, akilitangaza wakuu hao wapya wakati akizungumza na waandishi wa habari jana alisema 51 walioachwa inatokana na sababu mbalimbali za umri na utendaji wa kazi usioridhisha.
Aliwataja waandishi wa habari walioteuliwa ni Naibu Mhariri Mtendaji wa gazeti la Uhuru Publication Bi. Jacquline Liana ambaye pia aliwahi kuwa mhariri wa gazeti la Majira na Dar Leo.
Liana atakuwa mkuu wa wilaya ya Magu na Bw. Novatus Makunga (ITV Arusha) ambaye naye aliwahi kuandikia gazeti hili akiwa mwakilishi wa mkoa wa Arusha ambaye atakuwa mkuu wa wilaya ya Hai.
Aliwataja wengine kuwa ni watangazaji wa TBC Taifa, Bw. Selemani Mzee (Kwimba) na Bw. Selemani Kumchaya (Tabora), Bw. Ahmed Kipozi (Bagamoyo), Bw. Muhingo Rweyemamu (Handeni) na Bi. Lucy Mayenga ambaye pia aliwahi kuwa mwandishi wa gazeti hilo (Uyui) na aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya Majimaji ya Songea na mbunge wa Kilolo, Bw. Venance Mwamoto (Kibondo).
Kati ya wakuu hao wa wilaya watatu walipikwa na kuiva kitaaluma na Kampuni ya Business Times LTD inayochapishwa na magazeti ya Majira, Business-Times na Spoti Starehe na wengine watatu walipikwa na Redio Tanzania (RTD) sasa TBC-Taifa.
Waziri Mkuu Pinda aliwataja wengine kuwa ni Bw. Mboni Mgaza (Mkinga), Bi. Hanifa Serungu (Sikonge), Bi. Christine Mndeme (Hanang), Bw. Shaibu Ndemanga (Mwanga), Bw. Chrispin Meela (Rungwe), Dkt. Nassoro Ali Hamid (Lindi), Bi. Farida Mngomi (Masasi), Bw. Jeremba Munasa (Arumeru), Bw. Majid Hemed Mwanga (Lushoto), Bw. Mrisho Gambo (Korogwe), Bw. Eliasa Tarimo (Kilosa), Bw. Alfred Msovella (Kiteto).
Pia wamo Dkt. Leticia Warioba (Iringa), Dkt. Michael Yunia Kadeghe (Mbozi), Bibi Karen Yunus (Sengerema), Bw. Hassan Masala, (Kilombero), Bituni Msangi (Nzega), Bw. Ephraim Mmbaga (Liwale), Bw. Antony Mtaka (Mvomero), Bw. Herman Kapufi (Same), Bi. Magareth Malenga (Kyela), Bw. Chande Nalicho (Tunduru), Bi. Fatuma Toufig (Manyoni), Bw. Selemani Liwowa (Kilindi), Bi. Josephine Matiro (Makete), Bw. Gerald Guninita (Kilolo), Senyi Nganga (Mbinga), Bi. Mary Tesha (Ukerewe), Bw. Rodrick Mpogolo (Chato).
Waziri Mkuu aliwataja wakuu wa wilaya wengine wapya kuwa ni Bw. Christopher Magala (Newala), Paza Mwamlima (Mpanda), Bw. Richard Mbeho (Biharamulo), Bw. Joshua Mirumbe (Bunda), Bw. Costantine Kanyasu (Ngara), Bw. Yahya Nawanda (Iramba), Ulega Abdallah (Kilwa), Bw. Paul Mzindakaya (wilaya mpya ya Busega), Bw. Festo Kiswaga (Nanyumbu), Bw. Wilman Ndile (Mtwara), Bw. Joseph Mkirikiti (Songea), Bw. Ponsiano Nyami (Tandahimba).Bw. Elibariki Kingu (Kisarawe), Dkt. Charles Mlingwa (Siha), Manju Msambya (wilaya mpya ya Ikungi) na Bw. Omar Kwaangw (Kondoa).
Bw. Benson Mpesya (Kahama), Bw. Daud Ntibenda (Karatu), Bw. Ramadhani Maneno (Kigoma),Bi. Sauda Mtondoo (Rufiji), Bw. Gulamhusein Kifu (Mbarali), Esterina Kilasi (wilaya mpya ya Wanging'ombe), Bi. Subira Mgalu (Muheza), Bi. Martha Umbula (Kongwa), Bi. Rosemary Kirigini (Meatu), Bi. Agnes Hokororo (Ruangwa), Bw. Wilson Nkhambaku (Kishapu), Bw. Amani Mwenegoha (Bukombe), Bi. hafsa Mtasiwa (Pangani), Bi. Rosemary Senyamule (Ileje), Luteni Kanali Ngemela Lubisnga (Wilaya mpya ya Mlele), Bw. Idd Kimanta (Nkasi).
Wakuu wilaya 63 wa zamani waliobakishwa ni James Ole Millya (Longido), Mathew Sedoyeka (Sumbawanga), Fatuma Kimario (Igunga) Kepteni James Yamungu (Serengeti), Luteni Mstaafu Abdallah Kihato (Maswa), Bi. Sarah Dumba (Njombe), Jowika Kasunga (Monduli), Elizabeth Mkwasa (Bayi), Issa Njiku (Misenyi), Bw. John Henjewele (Tarime), Bw. Elias Lali (Ngorongoro), Bw. Raymond Mushi (Ilala), Bw. Francis Miti (Ulanga), Bw. Evarist Kalalu (Mufindi), Bi. Mariamu Lugaila (Misungwi).
Wengine ni Bi. Anna Magowa (Urambo), Bw. Anatoli Choya (Mbulu), Bi. Fatma Salum Ali (Chamwino), Bw. Deudatus Kinawilo (Chunya), Bw. Ibrahim Marwa (wilaya mpya ya Nyang'wale), Dkt. Norman Sigalla (Mbeya), Bw. Moshi Chang'a (wilaya mpya ya Mkalama), Bw. Jordan Rugimbana (Kinondoni), Bi. Georgina Bundala (wilaya mpya ya Itilima), Bi. Halima Kihemba (Kibaha), Manzie Mongochie (Geita), Bw. Abdula Lutavi (Namtumbo), Zipporah Pangani (Bukoba), Dkt. Ibrahim Msengi (Moshi), Kanali Cosmas Kayombo (wilaya mpya ya Kakonko), Lembris Kiputo (Muleba), Elinasi Pallangyo (Rombo), Queen Mlozi (Singida) Bw. Juma Madaha (Ludewa).
Wakuu wengine waliobaki ni Angelina Mabula (wilaya mpya ya Butiama), Bi. Hadija Nyembo (wilaya mpya ya Uvinza), Bw. Ernest Kahindi (wilaya mpya ya Nyasa), Bw. Peter Kiroya (Simanjiro), Bw. John Mongella (Arusha), Bw. Baraka Konisaga (Nyamagana), Bi. Husna Mwilima (wilaya mpya ya Mbogwe), Bi. Sophia Mjema (Temeke), Bw. Francis Isaac wilaya mpya ya Chemba), Bw. Abihudi Saideya wilaya mpya ya Momba, Bw. Khalid Mandia (Babati), Bi. Anna Rose Nyamubi (Shinyanga)
Pia wamo Dani Makanga (Kasulu), Bi. Amina Masenza (Ilemela), Bi. Mercy Silla (Mkuranga), Bw. Christpher Kangoye (Mpwapwa), Luteni Edward Lenga (wilaya mpya ya Kalambo), Bi. Halima Dendego (Tanga), Lephy Gembe (Dodoma), Bw. Said Amanzi (Morogoro), Bw. Jackson Msome (Musoma), Bw. Elias Goroi (Rorya), Luteni Kanali Benedict Kitenga (wilaya mpya ya Kyerwa), Gishuli Charles (wilaya mpya ya Buhigwe), Saveli Maketta wilaya mpya ya Kaliua na Darry Rwegasira (Karagwe).
mwisho
No comments:
Post a Comment