Jumamosi
ya tarehe 28 mwezi huu, Mtanzania Francis Cheka alinyakua ubingwa wa
"IBF Continental Africa" (ubingwa wa Africa wa IBF) katika uzito wa
Super Middleweight. Mpambano huo ulifanyika katika ukumbi wa PTA hapa
Dar-Es-Salaam. Bingwa Francis Cheka anatakiwa kutetea ubingwa huu katika
kipindi kisichozidi miezi sita (6)!
Mpambano
huu ulikuwa wa raundi 12 na kila raundi ilikuwa ni dakika tatu (3).
Promota wa Mpambano huu alikuwa Lucas Rutainurwa wa Kitwe General
Traders Limited ya Dar-Es-Salaam, Tanzania. Refarii alikuwa ni Bw.John
Shipanuka toka Zambia. Majaji; Bw. William Sekelete (Zambia), Bw. Simon
Katogole (Uganda) and Bw. Ismail Sekisambu (Uganda).
Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa (IBF) litapenda kuchukua fursa hii kumpongeza
bingwa Francis Cheka kwa kunyakua ubingwa wa Afrika.
Aidha
tunamtakia bondia Francis Cheka maisha mazuri kama bingwa na tunamuasa
aishi kama bingwa kwa kuonyesha nidhamu na uaminifu kama ubingwa wenyewe
unavyotakiwa kwani bingwa ni kioo cha jamii.
Tupenda
kuchukua fursa hii pia kushukuru sana vyombo vya habari pamoja na
waandishi mmoja mmoja kwa kazi nzuri sana waliyofanya wakati wote wa
maandalizi na siku ya pambano hili lilipofanyika. Kwa kweli vyombo vya
habari vimejenga hamasa kwa wapenzi wa mchazo wa ngumi hapa Tanzania na
Afrika nzima kwa jinsi walivyokuwa wana ripoti kwa hamasa kubwa.
Wakati
tukiwa kwenye somo hili la uandishi, viko vyombo vya habari na
waandishi ambao waliripoti kuwa huu ulikuwa ubingwa wa "IBF
Intercontinental", "IBF East Africa", "ubingwa wa IBF" n.k!
Tunapenda
kutoa taarifa sahihi kwa wapenzi wa ngumi kuwa hili lilikuwa pambano la
ubingwa wa Afrika (IBF Continental Africa Title) na sio mabara (IBF
Intercontinental Title) au sio ubingwa wa IBF wa Afrika Mashariki (IBF
East Africa)" au "ubingwa wa IBF wa dunia" (IBF Title).
Ni
vizuri tuwe tunatafuta taarifa au tafsiri sahihi kutoka kwenye vyombo
husika ili tusiikanganye jamii. Kwa hili pambano chombo husika ni IBF.
Tutapenda tena kurudia kwa kutoa shukrani zetu kwa vyombo vya habari pamoja na waandishi mmoja mmoja kwa kazi nzuri mlivofanya.
Mwisho,
tunapenda kurudia tena kumpongeza bingwa mpya wa "IBF Continental
Africa" Francis Ckeka kwa kunyakua ubingwa wa Afrika na tunamtakia
maisha mema na maandalizi mazuri ya kutetea taji lake katika kipindi cha
miezi sita.
You might also like:
No comments:
Post a Comment