TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday, 9 May 2012

ACT kushirikiana bega kwa bega na Vyombo vya habari

Na Peter Mwenda

BARAZA la Kilimo la Taifa (ACT)limeshauriwa kushirikiana na vyombo vya habari kutoa taarifa zinazohusu changamoto zinazokabili sekta ya kilimo nchini.

Wito huo umetolewa na washiriki wa semina ya waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kutolewa taarifa za kilimo kwa nanufaa ya Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa ACT, Bi. Janet Bitegeko alisema ushauri huo utafanyiwa kazi na kutakuwa na mafunzo na mikutano ya kupeana taarifa za maendeleo na changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo nchini.

Alisema kuna kasoro mbalimbali ambazo zinatakiwa kufanyiwa marekebisho ikiwemo Serikali kushindwa kutenga ardhi kwa ajili ya kilimo tofauti ilivyotenga kwa ajili ya wanyamapori na madini.

Bi. Bitegeko alisema kumekuwa na utitiri wa ushuru wa mazao kutoka shambani hadi sokoni hivyo kunufaisha wengine na kuwafanya wakulima waendelee kubaki masikini.

Katika mkutano huo mshauri wa Habari wa Kampuni ya Indigo-MTPC, Bw. Albert Msemembo alisema ushirikiano kati ya ACT na vyombo vya habari utakuza uzalishaji wa mazao kwa kusaidia kuondoa kero zinazowakabili wakulima na kuisadia serikali kujua changamoto zinazowakabili wakulima.

ACT yenye wanachama 123 kutoka vyama mbalimbali inatoa mafunzo ya kilimo, kusaidia kubuni mifumo ya kuinua kilimo ili kuondokana na uasikini.

mwisho

No comments:

Post a Comment