TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Thursday 19 April 2012

TASWIRA ZA MPAMBANO KATI YA YANGA NA KAGERA SUGAR KWENYE UWANJA WA KAITABA BUKOBA


 Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Fabian Masawe akikagua timu kabla ya kufanyika kwa mpambano wa ligi kuu ya Vodacom kati ya timu ya Yanga na Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jana ambapo timu ya Kagera Sugar iliikandamiza Yanga goli 1-0 na kutoka uwanjani kifua mbele.
Picha kwa hisani ya www.bukobawadau.blogspot.com
 Kocha wa timu ya yanga Bw. Kostadic Papic akiwa katika benchi la ufundi la timu hiyo na wachezaji wake kwenye uwanja wa Kaitaba jana.
 Wachezaji wa timu ya Yanga wakinywa maji wakati wa mpambano wao.
 Kikosi cha timu ya Kagera Sugar kikiwa katika picha ya pamoja.
 Mashabiki wa mpira wa miguu wakiwa wamefurika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba jana.
 Mmoja wa mashabiki anayesadikika ni mshabiki wa timu ya Simba akionekana kuwatania watani wake mashabiki wa timu ya Yanga
 Nyomi la mashabiki likifuatilia mchezo huo.
 Benchi la ufundi la timu ya Kagera Sugar.
picha na http://www.fullshangweblog.com/
Mdau MC  Baraka wa Bukobawadaublog kulia  akiwa na wadau wengine kwenye uwanja wa Kaitaba kushoto ni  Sadik Galiatano , Enock na mmoja wa mashabiki wa Yanga

No comments:

Post a Comment