TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Sunday, 22 April 2012

SBL WAJA NA SHUKRANI KWA WATANZANIA-VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO





  Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti (SBL) Epraim Mafuru (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi rasmi wa Promotion ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO kupitia bia tatu za Serengeti, Tusker na Pilsner Lager na washindi kujizolea zawadi mbali ambapo zawadi za Shilingi Milioni 700 kushindaniwa. Pamoja nae Kulia ni Mkuzaji wa M PESA kutoka Kitengo cha Biashara, Asia Natalia Mhina na Kushoto ni Meneja wa Bia ya Pilsner Lager, Maurice Njowoka.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Serengeti (SBL) Epraim Mafuru (katikati) akionesha zawadi mbali mbali zitakazo tolewa katika Promotion hiyo ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO kupitia bia tatu za Serengeti, Tusker na Pilsner Lager na washindi kujizolea zawadi mbali ambapo zawadi za Shilingi Milioni 700 kushindaniwa. Zawadi zitakazo tolewa ni pamoja na Fedha Taslimu, Bia za Bure, Jenereta, Bajaji, Pikipiki na Gari aina ya Figo. Mafuru amesema Promosheni hii itadumu kwa Wiki 16 kuanzia Jumanne Aprili 24,2012.
  Kulia ni Mkuzaji wa M PESA kutoka Kitengo cha Biashara, Asia Natalia Mhina. 

****
 
Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kupitia vinywaji vyake bora kabisa vya Serengeti premium Lager, Tusker Lager na Pilsner Lager iameandaa promosheni kubwa na ya aina yake itakayofanyika Tanzania nzima katika kipindi cha wiki 16 ambapo zawadi mbalimbali zitashindaniwa.

Promosheni hiyo ya aina yake imesheheni zawadi mbalimbali kubwa na ndogo kama vile Jenereta 16 , Pikipiki 8, Bajaji 8, Gari ndogo maarufu kama saloon car 8, pamoja na zawadi zingine nyingi ambapo kila baada ya wiki mbili gari 1  aina ya saloon itakuwa inashindaniwa, kila baada ya wiki mbili Bajaji 1 itakuwa inashindaniwa, kila baada ya wiki  Pikipiki moja itashindaniwa na kila baada ya wiki moja Jenereta moja itakuwa inashindaniwa.

Akizungumzia promosheni hiyo  kabambe Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, bwana Ephraim Mafuru  amesema  promosheni hiyo sio tu inalenga kuongeza mauzo ya vinywaji hivyo bali pia inalenga kuinua na kubadilisha maisha ya watanzania hususani wateja wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo ikiwa ni sera mojawapo ya kampuni hiyo kuisaidia jamii kwa njia mbalimbali kupitia bidhaa zake zenye ubora wa aina yake.

“Kampuni yetu imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo ya taifa letu katika maeneo mbalimbli kupitia jamii inayotuzunguka na wateja wetu kimaisha, hivyo promosheni hii pamoja na ukweli kuwa inalenga kuongeza tija katika masoko ya bidhaa zetu bado unaweza kuona zawadi zitakazoshindaniwa katika promosheni hii ni zawadi kubwa ambazo kwa namna moja ama nyingine inaweza kubadilisha maisha ya mshindi wetu kutoka hatua aliokuwepo hadi hatua nyingine, kwa hivyo sisi SBL tunasema tunajivunia kuwa sehemu mojawapo inayochangia maendeleo ya watanzania wateja wetu na taifa kwa ujumla” alisema bwana Mafuru. 

Kwa upande wake Meneja wa bia ya Tusker Lager, Bi Rita Mchaki, amesema kampuni ya bia ya Serengeti inazalisha bidhaa zinazopendwa na watanzania wengi kutokana na ubora wa kipekee wa bidhaa hiyo, na kwamba promosheni hiyo kabambe nisawa nakurudisha shukrani zake kwa watanzania kwa kufanikisha kampuni hiyo kufikia malengo yake kibiashara. 
Watanzania wote wenye umri wa miaka 18 na zaidi na wanaotumia bidhaa zetu zilizoainishwa katika promosheni hii wanaombwa kushiriki kwa wingi bila kukata tamaa kwani zawadi zinazoshindaniwa zinaweza kubadilisha maisha kwa yeyote atakayebahatika kuibuka na ushindi. 

MAELEKEZO:
Nunua bia ya serengeti lager, Tusker lager au Pilsner Lager fungua kisha bandua ganda lililo ndania ya kizibo utapata namba zilizopo katikati ya kizibo, Fungua sehemu ya kutuma ujumbe mfupi kwenye simu yako, nakili namba hizo mfano 55550, kisha tuma namba zilizopo pembezoni mwa kizibo. Fanya hivyo kwa kufuata maelekezo katika vipeperushi na magazeti.unaweza pia kijipatia bia ya bure papo hapo kila ubanduapo kizibo cha bia ziliainishwa katika promosheni hii.

No comments:

Post a Comment