TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday, 18 April 2012

Mwinyimsa mgeni rasmi chuo cha Uhazili Splendid

Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Mkoa wa zamani wa Mkoa wa Tabora, Bw. Abeid Mwinyimsa atakuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 24 ya Chuo cha Uhazili cha Splendid cha Ilala Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Splendid, Bw. Caasim Taalib alisema jana kuwa katika sherehe za mahafali hayo zitakazofanyika Ijumaa kuanzia saa 3.00 asubuhi Bw. Mwinyimsa atawawazawadia vyeti wahitimu 60 waliofaulu vizuri masomo yao.

Alisema Chuo cha Splendid ambacho kimesajiliwa na Mamlaka ya Ufundi Stadi Tanzania (VETA) mpaka sasa kimetoa wanafunzi zaidi ya 10,000 kutoka kianziashwe mwaka 1988 ni chuo pekee ambacho wanafunzi wake wamepata ajira na wengine kujiajiri wenyewe.

"Ninayo furaha kubwa kuona wanafunzi wangu wote waliopita chuo hiki wanarudi kushukuru kuwa wote wanafanyakazi za maana za kuajiriwa na wengine wamejiajiri" alisema Bw. Taalib.

Alisema Chuo cha Splendid kinatoa mafunzo ya uhazili kwa nadharia na vitendo kutumia teknolojia za zamani na kisasa katika kufundishia mabako ni vigumu mwanafunzi kushindwa kuelewa.

Bw. Taalib alisema chuo hicho pia kinatoa mafunzo ya Komputa (IT),biasshara wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya kufaulu Kidato cha Pili (QT),Wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita.

mwisho.

No comments:

Post a Comment