Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa (wa pili kulia) akiwa pamoja na
Askofu Mkuu wa Kanisa la EAGT,Askofu Keneth Kasunga katika ibada maalumu
wakati wa tafrija ya uchangiaji wa Ujenzi wa Kanisa hilo lililopo mjini Tunduma wilaya ya
Mbozi mkoani Mbeya,iliyofanyika kwenye viwanja vya Hoteli ya High Class
mjini humo.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akitoa hotuba yake wakati wa
hafla hiyo ya kuchaangia ujenzi wa Kanisa la EAGT lililopo mjini
Tunduma wilaya ya
Mbozi mkoani Mbeya.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akisalimiana na MC
Charles Mwakipesile ambaye pia ni mwandishi wa habari gazeti la Majira
mkoani Mbeya.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa (kushoto) akiagana na baadhi ya
viongozi wa kanisa hilo.Wa pili Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya,Mh.
Evance Balama.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiwapungia waumini wa Kanisa la
EAGT mara baada ya kuwahutubia wakati wa hafla ya uchangiaji wa ujenzi
wa kanisa hilo lililopo mjini Tunduma wilaya ya
Mbozi mkoani Mbeya.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akiongozana na Askofu Mkuu wa
Kanisa la EAGT,Askofu Keneth Kasunga pamoja na waumini wengine wa kanisa
hilo wakati wakitoka kwenye viwanja vya Hoteli ya High Class muda mfupi
baada ya hafla fupi ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo,lililopo mjini
Tunduma wilaya ya
Mbozi mkoani Mbeya.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari mara baada kumalizika kwa tafrija hiyo.
Na Mwandishi Wetu,Mbeya.
WAZIRI mkuu mstaafu,Edward Lowassa ametoa Shilingi Milioni 10 taslimu
kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la EAGT lililopo mjini Tunduma wilaya ya
Mbozi mkoani Mbeya.
Fedha hizo amezitoa wakati wa harambee ya kuchagia ujenzi wa
kanisa hilo ililofanyika katika viwanja vya Hoteli ya High Class mjini
hapa.
Lowassa ambaye alitumia takribani dakika 28 pekee kuwepo katika
viwanja hivyo, alisema kuwa watanzania ni vema wakawa na wito wa kujenga
nyumba za kuabudia kuliko kujenga nyumba za starehe zikiwemo Bar.
‘’Nafurahi kualikwa katika tafrija hii na niwaombe kwa pamoja tuwe
na tabia za kujenga nyumba za Mungu ambazo zitakusanya waumini kuabudia
na kuomba kwa pamoja kuliko hivi ilivyo wengi wanajenga Bar’’ alisema
Lowassa.
Aliongeza kuwa kwa sasa nchi ipo katika kipindi kigumu cha uchumi na
masuala ya katiba mpya hivyo aliwaomba wakristo kupanga ratiba ya
kuiombea nchi ili iendelee kuwa na amani na watanzania kuendelea
kuimarisha ushirikiano na umoja uliopo.
Alisema kuwa jambo hilo ni muhimu kwa kila mtanzania ambapo kila
mmoja aliombee taifa,ili lisikumbwe naghasia na mambo kama yale
yanayotokea katika nchi zingine ikiwemo Nigeria ambako kikundi cha Boko
Haramu hakiwataki Wakristo.
‘’Mimi ,familia yangu na marafiki zangu tumeguswa na ujenzi wa
nyumba ya Mungu na tunatoa Shilingi Milioni 10 na huu ni mwanzo tu’’
alisema Lowassa.
Sanjari na kutoa fedha hizo, pia alimuomba askofu wa kanisa hilo aandae tamasha
la kuchagia ujenzi huo kwa kwaya zote ambazo zilihudhuria harambee hiyo
na kwamba kwaya tatu zitakazoshinda zitachagua mwakilishi mmoja ambao
atawagharamia kwenda nchini Israel kuona historia ya kikristo.
Alisema amefanya hivyo kwasababu anapenda sana uimbaji na kwamba
alibarikiwa zaidi alipoimba pamoja na wanakwaya hao wimbo usemao ‘’Bwana
Mungu nashangaa kabisa nikitazama jinsi ulivyo……..
Kwa upande wake Askofu mkuu wa Kanisa hilo,Keneth Kasunga alimshukuru Waziri Mkuu huyo
mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Monduli kuwa amejenga
nyumba ya Mungu na wala si ya Mtu binafsi hivyo Mungu hawezi kumuacha
katika mambo yake yote na mahitaji pia.
No comments:
Post a Comment