TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Saturday, 14 April 2012

KUMBUKUMBU YA SOKOINNE / KUAPISHWA TUME YA KATIBA



Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Waziri Mkuu, Mstaafu, Edward Lowassa katika Ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye Kanisa Katoliki, Kigango cha Wami Sokoine, Morogoro Aprili 12,2012. Watatu Kushoto ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
Baadhi ya washiriki wa Ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine wakishiriki katika Ibada hiyo kwenye Kigango cha Kanisa Katoliki cha Wami Sokoine, Morogoro Aprili 12, 2012.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodluck Ole Mideye akishiriki katika ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye Kigango cha Kanisa Katoliki cha Wami Sokoine, Morogoro Aprili 12, 2012.
Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Mhasham Telsphor Mkude akibariki sanamu ya aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine kwenye viwanja vya Kikagango cha Kanisa hilo katika kijiji cha Wami Sokoine , Morogoro baada ya kuongoza Ibada ya kumkumbuka kiongozi huyo Aprili 12,2012.
Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Telsphor Mkude akiteta na Namelok Sokoine, Binti wa aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Moringe Sokoine ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum katika ibada ya kumkumbuka kiongozi huyo iliyofanyika kwenye Kigango cha Kanisa Katoliki cha Wami Sokoine,Morogoro Aprili 12,2012.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Askofu wa Jimbo Katoliki la Morogoro, Telsphor Mkude baada ya Ibada ya kumkumbuka aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Moringe Sokoine iliyofanyika kwenye kanisa katoliki, Kigango cha Wami Sokoine Aprili 12, 2012. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na watatu kulia ni Binti wa Marehemu Soine, Namelok Sokoine ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Makamu wa rais, Dkt, Mohamed Ghalib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika sherehe za kuwaapisha wajumbe wa Tume ya kuratibu Maoni ya Wananchi Kuhusu Kuundwa kwa Katiba Mpya zilizofanyika Ikulu jijini Dar es salaam Aprili 13,2012.
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya Kuratibu Moani ya Wananchi Kuhusu Kuundea kwa Katiba Mpya baada ya kuwaapisha, Ikulu jijini Dar es salaam, Aprili 13, 2012.

No comments:

Post a Comment