Bondia
Francis Cheka (kulia) akimsukumia konde mpinzani wake Mada Maugo,
wakati wa pambano lao lililokuwa la Raundi 12 lililofanyika katika
Ukumbi wa PTA usiku huu. Mada Maugo aliwashangaza mashabiki wa mchezo
huo pale alipoanza pambano hilo kwa spidi ya ajabu na kufanikiwa
kumpeleka chini mpinzani wake mara mbili katika raundi ya pili na ya
tatu, baada ya raundi ya nne mchezo ulibadilika na Mada kuanza kuelemewa
na kupoteza mwelekeo huku akikumbatia kila mara.
Ilipofika
raundi ya sita kabla ya kuanza raundi ya saba, Mada Maugo alitangaza
kutoendelea na mchezo kwa kile alichodai kuishiwa na pumzi huku
akisikika kusema, 'Sirudi Jamaa ataniua' huku akivua Glovz na kumpa
ushindi mpinzani wake wa Teknical Know Count TKO.
Baada ya mchezo huo alipohojiwa na mtandao huu
Mada alisema kuwa ilipofika raundi ya nne tu alikuwa hamuoni mpinzani
wake jukwaani lakini alijikaza na kuendelea kushambulia huku akishtukia
makonde yanatua usoni na ndipo ilipofika raundi ya sita aliamua
kumwambia msimamizi wake kuwa hawezi kuendelea na pambano hilo.
Mada Maugo, akimpeleka chini mpinzani wake Cheka.
Mashabiki wa Mada, wakishangilia...
Mada Maugo (kulia) akishambulia kwa konde zito.
Wakichapana kwa zamu...
Mada akishambulia....
Mashabiki wa ngumi wakishangilia pambano hilo.
Mashabiki wa Cheka, wakishangilia na kulizunguka gari alilokabidhiwa Cheka, baada ya kutangazwa mshindi.
Cheka
akisaidiwa na polisi baada ya kuzongwa na mashabiki wake wakitaka
kumbeba na kuzunguka naye ukumbini humo baada ya kushinda pambano hilo.
Nasib
Ramadhan (kushoto) akichapana na Moro Best katika moja ya pambano la
utangulizi, ambapo Nasib alishinda kwa KO katika Raundi ya nne.
Simba
wa Tunduru (kulia) akishangilia baada ya kumchapa mpinzani wake Mohamed
Kashinde kwa KO katika Raundi ya 6 Dakika ya 2 na Sekunde 59, huku
mohamed akiwa naongoza kwa mchezo bomba kabla ya kuangushwa.
Simba wa Tunduru, akishangilia kwa staili yake baada ya kumwangusha mpinzani wake.
Mgeni
Rasmi, Meya wa Ilala, Jerry Slaa, akiwa na baadhi ya viongozi wa mchezo
huo meza kuu wakifuatilia kwa makini mapambano hayo.
Mrembo, Elizabeth Pertty, akipita jukwaani kuonyesha namba za raundi ya pambano hilo.
Cosmas Cheka (kulia) akipambana na Sadick Momba. Katika pambano hilo Momba alishinda kwa Pointi.
No comments:
Post a Comment