TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Monday, 2 April 2012

Fani ya Ugavi, ununuzi inaongeza uchumi, Meya wa Bukoba

Na Peter Mwenda

MEYA wa Bukoba, Bw. Aman Anatory amesema fani ya ununuzi na Ugavi inajukumu kubwa katika uchumi kwa vile inahusika moja kwa moja katika kuinua uchumi.

Akizungumza katika mahafali ya tisa ya Chuo cha Ununuzi na Ugavi (IPS),Chanika Dar es Salaam juzi, Meya Aman alisema fani ya ugavi na ununuzi ndiyo husimamia matumizi mazuri ya fedha za walipa kodi.

"Fani ya ununuzi na ugavi ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi yoyote duniani,asilimia kubwa ya fedha za walipa kodi hutumika katika manunuzi ya mipango ya maendeleo ya nchi" alisema Meya Aman.

Alisema ni jukumu la wahitimu kwenda kuwadhihirishia waajiri kuwa ujuzi waliopata katika kozi hizo ni kwa ajili ya kuongeza ifanisi ili kunusuru fedha za umma zisiingie mifukoni.

Awali Mkuu wa Chuo cha IPS, Bw. Leonard Lyatuu alisema chuo hicho kutoka kianze kufundisha mwaka 2002 kimekuwa kikitoa kozi mbalimbali za ugavu na ununuzi nchini.

Alisema mwaka 2003, IPS walikubalika na Chuo cha CIPS (UK) cha Uingereza kinachosimamia mafunzo hayo na mitihani.

Alisema mpaka sasa Chuo cha IPS kina wanafunzi 354 katika kozi za ugavi na ununuzi.

mwisho

No comments:

Post a Comment