CUF – Chama Cha Wananchi kimeshtushwa na taarifa kwa vyombo iliyotolewa na Mgurugenzi Mkuu wa Idara ya Bohari ya Dawa Bw. Joseph Mgaya amenukuliwa akisema kwamba sababu kuu ya ongezeko la upungufu wa dawa kwenye zahanati na hospitali hapa nchini ni kutokana na ongezeko kubwa la mahitaji. Ambapo kwa tafsiri rahisi maanake ni ongezeko la wagonjwa kwenye hospitali hoja ambayo ni hafifu kabisa.
Serikali iantakiwa kujua idadi ya wagonjwa watakaongezeka kwa kipindi Fulani kutokana na takwimu wanazochukua kutoka hospitalizote Tanzania kwa hiyo hoja kwamba kunaongezeko la matumizi haina mashiko hata kidogo
Wakat i huo huo Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) imebaini “madudu” katika wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, baadaya ya kubaini hasara kaimu katibu wa wa wizara ya Afya bi.Regina Kikuli akitoa taarifa kwa kamati ya kudumu bunge ya Hesabu za Serikali (PAK) ilibainisha kwamba dawa zenye thamani ya zaidi ya bilionin 4.5 zimeharibiwa kutokana na kuisha muda wake wakati watanzania wengi wanalazimika kununua dawa kwenye maduka ama kukosa kabisa kulingana na maeneo kutokana na kukosekana kwa dawa kwenye hospitali na zahanati za serikali.
Madawa ya thamani ya bilioni 4.5 ni mengi sana lakini yanaharibika wakati watumiaji wapo wanayahitaji sana tena kunamaeneo hasa ya vijiji ambako maduka ya dawa ni tabu kuyapata watanzania wanakufa kwa kukosa hizo dawa.Lakini leo serikali ya CCM inaacha madawa yaishe muda isubiri kuyateketeza.
UONGOZI MSD USIMAMISHE KUPISHA UCHUNGUZI
Wizara ya Afya na inatakiwa kujibu maswali yafultayo;-
· Dawa gani zimeharibika?ili kujua kiwango cha magonjwa wanayoua watu kwa kukosekana kwa dawa Fulani.
· Mfumo wa ugawaji dawa kwenye hospitali na zahanati za Tanzania unakasoro gani.
· Wanaohusika na kasoro hizo ni kinanaini.
Tunaitaka serikali isimamishe mara maja mkurugenzi wa MSD weongozi waandamizi wote wanaohusika na hasara hii ili kupisha uchunguzi wa kubaini chanzo cha tatizo hili na wanohusika na hasa na tatizo hilo hihili.kisha wachukuliwe hatua kali za kisheria kwani watakuwa wanahusika na upotefu wa maisha ya watanznania wengi waliopoteza maisaha kwa kukosa dawa kwenye zahanati na hospitali.
Naibu Katibu Mkuu CUF-Julius Mtatiro
No comments:
Post a Comment