Na Peter Mwenda, Kisarawe
DIWANI wa Kata ya Vikumburu Bw. Juma Dihomba amekuja juu baada ya kuambiwa madiwani wa Halmasahauri ya Kisarawe mbumbumbu wakidaiwa kuidhinisha sh. mil. 500 kwa ajili ya elimu ambazo ni sawa na fedha walizoidhinisha kwa ajili ya kujenga nyumba ya Mkurugenzi na ununuzi wa gari la kifahari.
Wakitoa madai hayo watoa mada wawili, Bw. Peter Kibehi wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Mope na Bw. Bugi Ngeseni wa taasisi ya kwa pamoja waliwaambia washiriki wqa warsha hiyo kuwa madiwqani hao wameidhinisha sh. mil. 500 kwa ajili ya kuendeleza elimu ambazo hazitoshim kutokana hali halisi ya elimu duni itolewayo katika wilaya ya Kisarawe.
"Mimi nimesoma shule ya Sekondari Mwaneromango ambayo imesomesha viongozi wengi na wataalamu katika sekta mbalimbali akiwemo mbunge wa Kisarawe Bw. Suleiman Jafo lakini sasa shule hiyo imeshika nafasi ya pili kutoka mwisho katika matokeo ya kidato cha nne mwaka huu" alisema Bw.Bugi.
Bw. Bugi alisema wakurugenzi wamekuwa wakiunda kikundi cha madiwani wao ambao wanawaburuza katika vikao vya halmashauri kwa sababu ya elimu yao ni darasa la saba ambayo hawana uwezo wa kujenga hoja katika vikao vya halmashauri ambayo vinaandikwa kiingereza.
Katika warsha hiyo iliyoandaliwa na Kisarawe Development Foundation (KIDEFO) iliwalenga wananchi wa Kata ya Msimbu, Msanga,Asasi za kiraia na makundi maalum, Mbunge wa Viti Maalum Walemavu Mkoa wa Tanga, Bi. Al Shalmaa Kwegyir alisema elimu ya uraia na utawala bora unasaidia wananchi kujiamini katika kuchangia maendeleo yao.
Naye Diwani wa Vikumburu Bw. Dihonga kupitia Chama cha Wananchi (CUF) alisema amekubali maoni ya wananchi wa Kisarawe na kuahidi kubadili mwelekeo wa kuongeza wigo katika halmashauri kuwa hatakuwa tayari kuwa kiongozi wa kupitisha bajeti ambayo haina manufaa kwa wananchi wa Kisarawe.
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Jinsia wilayani hapa, Bibi Gretude Mwanakadudu alisema anafurahi kuona wananchi wa Kisarawe wanazinduka na kuitaka maendeleo katika wilaya hiyo ambayo ina historia kubwa nchini.
Bibi Manakadudu alisema amewahi kupata taarifa kuwa wenyeji wa wilaya ya Kisarawe waliwahi kutakaa isijengwe hospitali ambayo ndiyo ilikwenda kujengwa mkoa wa Kilimanjaro ya KCMC kwa imani za kidini.
Mwenyekiti wa KIDEFO, Bw.Haroun Hamisi alisema warsha hiyo ni ya pili kufanyika kwa ajili ya kuwajengea uwezo wananchi wa kawaida, viongozi wa ngazi za vitongoji,Kata na wilaya ya Kisarawe.
Bibi. Monica Mahoza alisema tatizo la elimu kwa madiwani wa Kisarawe ni kubwa kwa vili waliomaliza kidato cha nne na sita ni wachache hivyo kazi ya kuchanganua bajeti ya halmashauri inakuwa ngumu.
mwisho
No comments:
Post a Comment