TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday, 29 February 2012

Benki ya Afrika yazawadia washindi wa riadha Bamako

Na Peter Mwenda

BENKI ya Africa Tanzania imetoa zawadi mbalimbali kwa mwanariadha, Sarah Kavina aliyepeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mashindano ya mbio ya kimataifa  yaliyofanyika hivi karibuni Bamako, nchini Mali.

Akizungumza kabla yakuwakabidhi zawadi ya pesa taslimu, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Africa Tanzania, Ammish Owusu-Amoah alisema benki yao iliwapeleka wachezazi wawili wa Tanzania,Sarah Kavina na Andrea Mathiya ambao wamefanya vizuri.

“Tunayofuraha kuwajulisha kuwa, Sarah Kavina aliibuka kwa kupeperusha bendera ya Tanzania vyema katika mashindano ya kimataifa ya benki Afrika "Bank of Africa International Marathon’ ya kilomita kumi kwa upande wa wanawake ambapo nchi 14 zilishiriki ikiwemo nchi ya Ufaransa,”alisema,Owusu-Amoah.

Alisema mashindano hayo hushirikisha nchi ambazo benki hiyo inafanya kazi ambapo Tanzania ilishiriki kwa awamu ya pili na imeweza kupata ushindi kwa upande wa mbio za wanawake kwa awamu zote kupitia mwanariadha Sarah .

Alisema benki pia limpatia zawadi Andrea Mathiya kwa kushiriki kwake vizuri katika mashindano hayo lakini hakurudi na ushindi na kumtaka kuzidi kufanya vizuri katika mchezo huo ili mwaka ujao aweze kushiriki tena na kupata ushindi.

Alisema Benki yao itazidi kuwaandaa watanzania kama njia ya kusaidia kuibua na kukuza vipaji katika mchezo huo ili waweze kushiriki hata katika mbio za kimataifa zikiwemo za Olimpiki.

Mkuu wa Shughuli Kibiashara za Kibenki,Wasia Mushi alisema mashindano  waliyoshirki wanariadha katika mashindano hayo ni  kilomita 42 kwa wanaume walio na umri wa miaka 18 na kuendelea, kilomita kumi kwa wanawake wenye umri wa miaka 18 na kuendelea, kilimomita tano kwa wasichana chini ya miaka 18 na wavulana chini ya miaka 18.

Alisema benki iliwapeleka wanariadha wa mbio za kilomita 42 kwa wanaume na kilomita 18 kwa wanawake na waliweza kushiriki vizuri na kubahatika kurudi na ushindi kwa upande wa wanawake ambao umetoa hamasa kubwa kwa wanamchezo huo kuzidi kufanya vizuri katika mashindano mengine.

Naye  Sarah  aliishukuru benki hiyo kwa kuwawezesha kushiriki mashindano hayo yaliyowapatia mbinu, ujuzi na hamasa kubwa katika tathinia ya mchezo huo mabao unaushindani mkubwa.

“Mimi nilishinda kwa upande wa wanawake kutoka nchi zote zilizoshiriki na mwezangu wa Tanzania, Andrea kwa upande wa wanaume katika mbio za kilimota 45 alikuwa akiongoza lakini kabla ya kumaliza aliumia na kushindwa kurudi na ushindi,”.

Alisema  benki hiyo iliwandaa vizuri kuanzia hatua ya mazoezi,vifaa na  malazi na kuwafanya kuwa washindani wazuri na kufanikiwa kuipeperusha bendela ya taifa na kufanikiwa kurudi nyumbani na

Alisema anaiomba benki hiyo kuzidi kuwafadhili kwa hali na mali katika mashindano hayo kwani wao wapo tayari katika masindano mbalimbali na kuiletea heshima nchi yao katika mchezo huo unaopendwa na watu wengi duniani.

Alikiomba Chama cha Riadha Tanzania (RT) kuiga mfano wa benki hiyo katika maandalizi ya mchezo huo ili washiriki warudi na ushindi katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. 

Mshindano hayo yalianzishwa mwaka 2009 na Bank of Africa ambayo hufanyika kila mwaka kwa nchi ambazo benki hiyo inafanykazi kama njia ya kuleta mahusiano mema na njamii na kukuza vipaji vya wanamichezo wa nchi hizo.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment