TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday, 11 November 2011

Mlima Kilianjaro uko Tanzania si Kenyaa asema Balozi wa Kenya nchini

Na Peter Mwenda

SERIKALI ya Kenya imewahakikishia watanzania kuwa Mlima Kilimanjaro unaoingizwa kwenye vivutio saba vya dunia ni mali ya Tanzania.

Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Bw. Mutinda Mutiso akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa nchi saba wanachama wa mkataba wa Lusaka wa kupambana na ujangili unaofanyika Dar es Salaam na Tanzania kuwa mwenyeji alisema anawapongeza watanzania kuwa na kivutio kikubwa kama hicho na nchi yake itasaidia kuutangaza mlima huo.

"Kenya inawapongeza watanzania kuwa na mlima wenye historia kubwa kama Kilimanjaro, wakenya wanafahamu kuwa si mali yao na tunaahidi kuutangaza kuwa ni mali ya Tanzania" alisema Balozi Mutiso.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Bw. Ezekiel Maige akifungua mkutano wa kumi wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa Mkataba wa Lusaka wa kushirikiana katika mapambano ya kuzuia biashara haramu ya wanyamapori na mimea alisema katika kipindi chake cha miaka miwili ya kuongoza ushirikiano huo Tanzania imepata faida kubwa ya kupambana na majangili.

Alisema katika mkutano huo utajadili mbinu mbalimbali za kisasa za kupambana na majangili unafanyika wakati changamoto za ujangili na biashara haramu ya wanyamapori hasa tembo na faru zimeongezeka katika bara la Asia pia utatoa maamuzi muhimu yatakayoboresha utekelezaji wa mkataba

Waziri Amige alisema mkutano huo ambao mada kuu itahusu changamoto na fursa ya uhifadhi wanyamapori barani Afrika na kuongeza ushirikiano na utengamano, utanufaisha Tanzania kupambana na ujangili.

Nchi wanachama watakaohudhuria mkutano huo ni Congo (Brazzaville),Kenya, Lesotho, Liberia, tanzania, Uganda na Zambia na nchi za Ethiopia, Afrika Kusini na Swaziland ni washiriki ambao bado hajaridhia mkataba huo.

 Ofisa Mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP) Bi. Margaret Oduk alisema nchi wanachama wanatakiwa kuweka mikakati ya kuhakikisha maliasili na nyara za seikali za nchi husika hazichezewi na kuhatarisha viumbe vyenye hisoria kubwa duniani.

Mkurugenzi wa Kikosikazi cha Azimio la Lusaka, Bw. Bonaventure Ebayi wa Zambia alisema ushirikiano huo umesaidia kupunguza ujangili na maliasili nyingi zimekamatwa kwa wananchi wanachama wamepata nguvu ya kulinda maliasili zao.

mwisho

No comments:

Post a Comment