Na Stephano Samo, Hanang
WATU watatu wameumwa na fisi katika Kata ya Mogitu wilaya ya Hanang mkoani Manyara wakati wakinywa pombe klabuni.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mogitu
Bw. Sencer Machagwa akizungumza na Majira juzi alisema fisi huyo amewauma watu hao katika maeneo tofauti baada ya kuonekana eneo la Sabaradaqallu.
Alisema baada ya fisi huyo kuonekana eneo hilo hakuweza kumdhuru mtu ila ilipofika saa moja usiku aliwashambulia watu wawili katika maeneo ya Qatamohoga.
Bw. Machagwa alisema watu waliumwa na fisi huyo ni Bw.Sipu Qamu na Bw. Boay Salit ambao ni wakazi wa Dumbeta na mwingine ni Bw. Ginasaki
Qwasno mkazi wa Mogitu na wote wamelazwa hospitali kwa matibabu.
Alisema Bw. Qwasno amelazwa katika ya hospitali ya Dareda na Bw. Sipu na Bw. Boay wamelazwa katika hospitali ya Hyadom wilayani Mbulu.
Bw. Machagwa alisema fisi alionekana kwa mara ya kwanza saa nane mchana alipowatimua watu waliokuwa wanachota maji bombani na kuingia kunywa maji baada ya watu wote kukimbia na baada ya kutoka hapo aliingia vilabuni na kuwauma watu waliokuwa wanakunywa pombe.
Daktari wa Mifugo na Kilimo wilayani Hanang,Bw. Masaga Shushuda
aliiambia majira kuwa wananchi wangefanikiwa kumkata fisi huyo na kupimwa kubaini kama alikuwa na kichaa au la ila anawasiwasi kuwa fisi huyo atakuwa kichaa na kuishauri serikali ya kijiji kumtafuta na kumuua.
Alisema fisi huyo bila ya kuawa atawamaliza watu kwani atakuwa amelishwa sumu kali na ndicho kinachomsumbua"alisema Bw. Shushuda.
Wakazi wa kata hiyo wakizungumzia
tukio hilo walisema serikali ijipange kutoa tiba kwa watu wanaopata madhara ya kuumwa na wanyama.
mwisho
No comments:
Post a Comment