Na Mwandishi Wetu
KATIBU mkuu wa CCM, Bw. Wilson Mukama amekutana na Balozi wa Ujerumani nchini Bw. Klaus-Peter Brandes katika ofisi ndogo ya Makao makuu, dar es salaam.
Katika mazungumzo hayo Balozi Blandes alimhakikishia Bw. Mukama dhamira ya nchi yake kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuwapa maendeleo bila kujali itikadi zao za vyama vya siasa.
Hata hivyo Mukama alimwambia balozo huyo kuwa kupungua kwa idadi ya madiwani na wabunge wa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2010 kulitokana na makosa ya kuteua wagombea wasiokubalika kwa wapiga kura kwani wengi wa hao walipohamia upinzani walishinda.
Bw. Mukama alisema kama ilivyo kwa Ujerumani itapendekezwa kuondokana na chaguzi ndogo kutokana na kuwa na gharama kubwa kwa serikali na vyama vya siasa vinavyoshiriki pindi inapotokea nafasi ya mbunge na diwani kuwa wazi.
mwisho.
No comments:
Post a Comment