TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Sunday, 16 October 2011


“Upepo wa mapinduzi uliwaathiri sana wawekezaji ambao walikuwa wapo Libya kwa kupitia mgongo wa Mfalme Idris wa Kwanza , kwani licha ya shughuli zao kusitishwa na kanali Gaddafi ,"

"Pia shughuli zote zilitaifishwa zikiwamo sekta za uchumi, viwanda, shughuli zote ambazo zilikuwa zinahusiana na viwanda vya mafuta zikiwamo sekta nyingine muhimu,”alikaririwa mwanaharakati mmoja.

Kutokea hapo baada ya Kanali Gaddafi kukaa madarakani kwa kipindi cha miaka kadhaa alianza kuwavurumisha wawekezaji na wageni wa kizungu toka mwaka 1972.

Baadhi ya Mashirika ya habari ndani na nje ya Libya yanaeleza kuwa maamuzi hayo  ya Kanali Gaddafi, yalipelekea kuvifungia viwanda vyote vya kutengeneza pombe  na kuvitaifisha, ambapo mwaka 1973 alivichukua viwanda vyote vya mafuta ili kuwa chini ya  miliki ya serikali,

“Mfumo huo na maamuzi hayo yaliifanya Libya kuchukiwa na hata kutengwa na mataifa mbalimbali,” unafafanua mtandao wa answers.com.

Mtandao huo unafafanua kuwa  kuchukiwa huko,Kanali Gaddafi aliona siyo sababu  ndipo akaamua kuunganisha nguvu  kwa kuyaunga mkono makundi ya kigaidi ili yaweze kufanya  mashambulizi Ulaya na nchi nyingine na kuanza kuyaunga mkono baadhi ya makundi ili yaweze kufanya mapinduzi katika mataifa mengine.

Baada ya kukamilisha mikakati yake ya awali ya mapinduzi na mabadiliko katika kuwasafisha maadui ambao aliona ndi waharibifu wa uchumi wa Libiya.

KanaliGaddafi mwaka  1975 aliamua kuandaa falsafa za utawala wake kwa kuandaa kitabu maalum cha kijani (Green Book) ambacho kilijikita katika falsafa za kisiasa, uchumi na utawala wa ujamaa.

Kwa mujibu wa wanaharakai wanasema kwamba kupitia ‘falsafa ya ulimwengu wa tatu’ katika kitabu chake cha Kijani(Green Book), Kanali Qaddafi aliweza kuijenga Libya kuanzia nyanja za kisiasa, uchumi, mfumo wa ulinzi imara wa kijeshi.

Kufanikiwa kuanzisha na kuiendesha Jamahiriya ya watu walibya, miundombinu bora, ujamaa na utawala wa watu wa kushiriki katika maendeleo moja kwa moja toka 1975  na kuebdelea.

    Kitabu: kauli za Gaddafi

Dhumuni kubwa la kitabu cha kijani, kanali Gaddafi anasema ni kuelimisha wapinzani  ili waweze kutambua nafasi na namna ambavyo mahitaji ya walibya kupitia mfumo wa ujamaa yanavyotekelezwa.

Green Book ni kitabu kidogo ambacho kinaelezea kwa undani juu ya masuala ya siasa  za Libya  kikilenga kuwafikia walibya wote ili waweze kukisoma na kifahamu kile ambacho  wanapaswa kufanya na yale  ambayo walipaswa kuyapuuza kutoka kwa maadu ili waweze kupiga hatua za kimaendeleo.

Kitabu hicho ambacho kimeandikwa kwa lugha nyepesi yenye kueleweka na wananchi mbalimbali  hususan lugha ya kiharabu na kiingereza kimeambatanishwa na nukuu mbalimbali ambazo zinatia hamasa  ya usomaji.

Ambapo kilifanikiwa kusambazwa ndani na nje ya nchi, inasadikika kwamba toka vita vya kumuondoa madarakani kanali Gaddafi maelfu kwa maelfu ya nakala za kitabu chake hicho zimechomwa na  waasi ili kupoteza kumbukumbu za kitabu hicho kuenziwa.

Kwa mujibu wa wanaharakati wanasema kwamba kitabu hicho kutokana na uzito wake ndani ya taifa la Libya toka kitungwe  watoto  nchini humo huwa wanatumia masaa mawili kila  wiki, kujifunza kitabu hicho kama sehemu yao ya mitaala ya masomo
Huku  kikitangazwa kila siku  katika vituo vya television na redio, licha ya kwamba taratibu za kuelezea kitabu hicho zinapatikana katika mbao mbalimbali kubwa za matangazo   nchini humo.

Kitabu hicho ambacho kimegawanyika katika sehemu kuu tatu  kina kurasa 110 huku kila ukurasa ulioandikwa kwa lugha nyepesi ukiwa na maneno mia mbili.

Moja wapo ya mambo ya msi ngi katika kitabu hicho yaliyoainishwa ni pamoja na suluhisho la matatizo ya demokrasia na utawala wa watu (kilichapwa mwanzoni mwa 1975).

Shemu ya pili ya kitabu hicho kinaelezea kwa undani juu ya Suluhisho la  changamoto zinazokumba sekta ya uchumi kupitia mfumo wa ujamaa  ambacho kilipigwa chapa mwaka  1977.

Sehemu ya tatu ya kitabu chake ambacho kilipigwa chapa Septemba , 1981 ambacho kinaeleza kwa kina juu ya misingi ya ya jamii hususan uwajibikaji na utekelelezaji wa wajibu kwa kufuata nadharia ya kimataifa .

Suala la kwanza ni pamoja na msimamo wake ambao anasisitiza kwamba  kwa kuwa wanawake huwa wanateseka zaidi katika jamii kutokana na ubebaji wa uchungu ni lazima wapewe fursa ya kiutendaji ndani ya taifa ilikuwarejeshea matumaini.

 "Wanawake, kama watu, ni binadamu, huu ni ukweli usiopingika... Wanawake ni tofauti na watu katika mfumo wamaisha kwa sababu ni wanawake,ukiangalia hata katika  ufalme wa mimea na wanyama wanawake wote wana umuhimu tena wa pekee tofauti na wanaume wana upee wao na nafasi yao pia,” anasema Kanali Gaddafi.

Anasema katika kitabu hicho cha kijani kwamba kwa mujibu wa Uzazi wanawake, ni tofauti na wanaume, kwani wao uvunja ungo kila mwezi  na hata uzoefu wa kubeba mimba  huku akinyoyesha kwazaidi ya miaka miwili kinyume kabisha na wanaume hivyo ni wajibu wa kila jamii kumrejeshea heshima mwanamke na  hata kupewa kipaumbele.

Kanali Gaddafi katika kitabu chake hicho anaendelea kusema kuwa  kila  jambo lina mwanzo na mwisho wake kwani miaka nenda rudi Afrika ilitawaliwa na rangi nyeupehadi kufikia hatua ya kupoteza taswira hivyo basi ni zamu ya waafrika nao kujitawala.

. "Kuna mzunguko katika  historia ya kijamii kwani  utawala wa mbio za njano wao waliona ni manufaa kwao kupitia  dunia, wakati walikuja kutoka Asia rangi nyeupe ya majaribio katika maeneo  ya utawala wengine wakatokea Magharibi hadi kufikia mabara yote kuingia Afrika, waliweza lakini sasa basi,sasa ni zamu ya watu weusi kupiga mbio za kiutawala katika dunia, " anasema Kanali Gaddafi.

Anasema maisha ya kila siku haiwezekani mtu mmoja kujimilikisha rasilimali ambazo  zinaziba nafasi kwa wengi kupata mafanikio huo utakuwa siyo mfumo stahiki wa kudumisha demokrasia na ujamaa kwa kuwa watu wote wana haki  za asili za kujieleza kwa njia yoyote ile haijalisha hata kama muhusika ni mwendawazimu ni lazima apewe nafasi.

“Watasema sana lakini, yote yanayosemwa yanatokana na maneo ya kizushi, ukweli ni kwamba kila mmoja ana haki ya kumiliki mali sawa, ujamaa kupitia demokrasia na haki ya kusema, lazima elimu ipatikane kwa taratibu za kufuata mfumo wan chini yetu kila siku haijalishi, hatuwezi kuendeshwa kwa kusahau uhalisia wetu ndiyo maana tukiwapa nafasi sana watakuwa wanatuendesha,” anasema Kanali Gaddafi.

Hasira za Marekani dhidi ya Gaddafi

Hali iliyoifanya Marekani kuchukia,kupitia  rais wa wakati huo, Bw.Ronald Regan akaamua kuagiza mashambulizi ya kumuangamiza Kanali Gaddafi  kupitia ndege maalum mwaka 1986, mashambulizi ambayo yalifanya milipuko sehemu za nchi hiyo yakiwemo makazi ya Gaddafi bila kumuua.

No comments:

Post a Comment