TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Saturday, 22 October 2011

NDEGE YAANGUKA ARUSHA,YAUA RUBANI

NDEGE ndogo yenye namba 5H/QTE iliyokuwa na watu wawili imeanguka katika eneo la Kijiji cha Samaria wilayani Arumeru na kuua mtu mmoja.

Ndege hiyo mali ya World Quality Travel and Tourism ya jijini Arusha ilikuwa ikitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea Arusha.

Akitoa taarifa`kwa vyombvo vya habari jana mjini hapa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Akili Mpwapwa alisema kwamba, ndege hiyo inadaiwa kuanguka Saa 1: 46 jioni mara baada ya kushindwa kutua kwenye uwanja mdogo wa Arusha kutokana na kutanda kwa giza kwenye uwanja huo.

Kaimu Kamanda aliwataja watu waliokuwa ndani ya ndege hiyo kuwa ni Rubani Ali Harun (24) pamoja na Lilian Koima, ambapo alimtaja mtu aliyepoteza maisha yake kuwa ni Harun wakati Liliani akijeruhiwa vibaya na kupelekwa
hospitali ya KCMC mjini Moshi.

“Tarifa`tuliyoipata inaeleza kuwa baada ya watu hawa kushindwa kutua kwenye uwanja mdogo wa Arusha walilazimika kugeuka na kwenda Uwanja wa Kilimanjaro (KIA) ili kuomba kutua huko.

“Hata hivyo wakiwa angani wanaelekea KIA gafla mawasiliano yao na muongoza ndege pale KIA yalipotea hatua iliyosababisha wao kupotea hadi pale ilipobainika kuwa ndege yao ilikuw ameanguka katika kijiji cha Samaria,” alisema Kaimu Kamanda Mpwapwa.

Akianisha vitu vilivyoharibika alisema, ndege yenyewe iliharibika vibaya huku kibanda cha mkazi wa Kijiji cha Samaria nacho kiliiharibiwa pamoja na mbuzi watatu walipoteza maisha baada ya ndege hiyo kuwaangukia.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment