Na Peter Mwenda
WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imezindua mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi wake kupandishwa vyeo na kujifunza mabadiliko yanayotokea duniani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule alisema mafunzo hayo ambayo ni kwa ajili ya maofisa waandamizi kwa ajili ya kuboresha utendaji wao wa kazi.
Alisema baada ya mafunzo hayo maofisa hao watakuwa wameboresha utendaji wao wa kazi utakaendana na ushindani wa kimataifa katika balozi za Tanzania katika nchi mbalimbali duniani.
Bw. Haule alisema programu hiyo ambayo ilisimama mwaka 1995, imeanzishwa tena katika chuo hicho ili kusaidia kuboresha utendaji wa kazi na kuingia katika nafasi ya maofisa wa ngazi za juu.
Alisema Chuo cha Diplomasia kitachangamoto kubwa ya ufinyu wa bajeti na inahitajika kutumia wataalamu ili kuijiendesha kwa ufanisi mkubwa.
Alisema katika sekta ya mambo ya nje kunahitajika wataalamu wa kutosha kutoka Zanzibar na Tanzania Bara na kuahidi kukabiliana na soko la mahitaji la wafanyakazi wa Wizara hiyo.
Naye Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Balozi Dkt. Mohamed Mahundi alisema programu hiyo imelenga kuwanoa wafanyakazi wa wizara hiyo kuwa vioo katika kukabiliana na mageuzi ya kimataifa ya kutatua matizo ya mbalimbali ya ugaidi wa kimataifa, uharamia na tabia nchi.
Alisema wakati Tanzania inatimiza miaka 50 ya uhuru wizara hiyo itapata picha ya mafanikio na kujipima kwa kuangalia mafanikio ya wizara hiyo kwa maofisa wao katika nchi mbalimbali duniani.
mwisho
No comments:
Post a Comment