TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday, 25 October 2011

Cheyo amhenyesha Kaimu Mkurugenzi TBS

Na Peter Mwenda

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeitaka Wizara ya Viwanda na Biashara ieleze kwanini imedharau azimio la Bunge la Jamhuri ya Muungano la mwaka 2009 lilitaka ukaguzi wa magari nje ya nchi usitishwe ili kuokoa fedha nyingi zinazopotea kwa ujanja ujanja.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw. John Cheyo alisema jeuri ya kudharau bunge imetoka wapi na kufanya ukaguzi huo uendelee na kuingizia Tanzania hasara kubwa inayozidi mara mbili ya bajeti ya wizara hiyo.

"Ukaguzi unaofanywa kwa magari yanayoagizwa Tanzania kutoka nje ya nchi ni wizi,unapeleka chasisi namba bila kukaguliwa unapewa setifiketi bila kukaguliwa na unamlipa tajiri mmoja bila kufanya ukaguzi"alisema Bw. Cheyo.

Pia Kamati hiyo imetakiwa ibuni njia nyingine ya kufanya katika soko la Afrika Mashariki badala ya kuweka vizuizi na vibali hiyo inawabughudhi wafanyabiashara na kuondoa maana ya biashara huria katika soko la Afrika Mashariki.

"Hivi karibuni tumeshuhudia matatizo ya sukari kuvushwa usiku kwa njia ya magendo, hilo neno magendo limekwisha siku nyingi kama majirani wanataka sukari yetu pelekeni na wao walete bidha inayozalishwa kwao" alisema Bw. Cheyo.

Bw. Cheyo aliagiza Tume ya Ushindani ikutane mara kwa mara kwa ajili ya kutafuta njia mbadala ya kufanya biashara yenye tija kwa wakulima.


Wizara hiyo ijue kuwa tabia ya kuzuia watu kufanya biasha imepitwa na wakati hivyo serikali inatakiwa kusaidia wananchi ili kuendana na ushindani wa soko la pamoja na Afrika Mashariki.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw. Joyce Mapunjo akijibu hilo alisema Wizara imeagiza tani 120 ya sukari kukabiliana na uhaba huo na kuongeza kuwa ili kuendana na ushindani wa kibiashara Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB) imekubali kutoa mkopo wa kujenga masoko mipakani.

Kaimu Mkurugenzi TBS, Bw. Leandri Kinabo alieleza Kamati hiyo kuwa shirika lake linafanya kazi kwa karibu na Wizara ili kuangalia njia ya kufuta ukaguzi wa magari ya nje.

Katika Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) imezikataa hesabu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa sababu kimetumia fedha nyingi bila kupata kibali cha Wizara ya Fedha.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Bw.Murtaza Mangungu alisema TIC imekiuka kwa kushindwa kupeleka mapendekezo ya matumizi ya fedha badala yake walijiamulia kutumia fedha bila kupata baraka za Msajili wa Hazina.

Alisema uwekezaji bado yaujawanufaisha wananchi hivyo TIC inatakiwa kushiriki moja kwa moja kwa manufaa ya wananchi katika maeneo ya uwekezaji.

Alisema TIC imeshindwa kupunguza gharama za uendeshaji wa kituo kulinganisha na shughuli wanazozifanya.

Alisema maeneo ya uwekezaji yashirikishwe mwananchi katika eneo husika na ujulishwe atakavyonufaika na uwekezaji huo na si kutumia nguvu.

"Matumizi ya TIC yamepanda kwa Sh. mil. 800 kwa mwaka 2010, mfano katika idara ya utawala matumizi yamekuwa makubwa sana, wanapoandaa mishahara na posho lazima Bodi iombe kibali cha Msajili wa Hazina, mfano usafiri imetoka sh. mil. 62 hadi sh. mil.168"alisema Bw. Mangungu.

No comments:

Post a Comment