Na Peter Mwenda
MBUNGE wa Jimbo la Kilwa Kusini kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Bw. Selemani Bungala maarufu wa jina la Bwege ameshinda kesi aliyofunguliwa na Ramadhani Madabida kupinga ushindi wake.
Taarifa kutoka kwa Naibu Mkurugenzi wa Siasa na Uchaguzi wa CUF, Bw. Shaweji Mketo aliyekuwepo mahakamani hapo alisema katika hukumu hiyo kesi hiyo imetupiliwa mbali na mlalamikaji anayo nafasi ya kukata rufaa.
Alisema hukumu hiyo iliyosomwa Jaji Fatuma Msengi wa Mahakama Kuu Kanda ya Kusini kituo cha Mtwara ilichambua kipengele kimoja hadi kingine na kuonekana mlalamikiwa hana kosa na kufanya kiti chake cha ubunge kitenguliwe.
Bw. Mketo alisema katika hukumu hiyo mlalamikiwa ambaye ni mbunge wa Jimbo la Kilwa alidaiwa kuwa wapiga kura waliompa ushindi hawakuwa na sifa za kupiga kura kwa sababu hakuwemo katika orodha ya majina watu wenye sifa hizo.
Hakimu Msengi alichambua madai hayo alisema madai mengine ni kuwa mlalamikiwa Bw. Bwege anadaiwa kusema kutangaza katika mikutano ya kampeni kuwa mlalamikaji Bw. Madabida si mkazi wa Kilwa hakuna ushahidi huo.
Bw. Mketto alisema baada ya Jaji Fatuma kutupilia mbali madai hayo mlalamikiwa Bw. Bwege anajiandaa kufungua kesi ya kudai fidia ya kesi sh. mil. 250 ikiwa ni gharama ya kuendesha kesi hiyo.
CUF ambacho kina mbunge mwingine wa Jimbo la Lindi Mjini Bw. Salum Barwani ambao wanafanya jumla ya wabunge wa Tanzania Bara kuwa wawili na Tanzania Visiwani 22 na kumi wa viti maalum.
mwisho.
No comments:
Post a Comment