TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday, 27 September 2011

Damu Salama yatangaza vita kwa watumishi wanaouza damu

Na Peter Mwenda

MPANGO wa Taifa wa Damu Salama umetangaza vita dhidi ya watumishi wa hospitali wanaojihusisha na biashara ya kuuza chupa za damu kwa wagonjwa au ndugu wa wagonjwa kutoa taarifa kwa njia ya simu au kufika vituo vya damu salama.


Kwa mujibu wa taarifa yaMeneja Mpango waTaifa Damu Salamu, Dkt. Efesper Nkya anasema jana kwamba kitendo cha uzaji wa damu katika hospitalini kinachofanywa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu kuna athiri kwa kiasi kikubwa uhamasishaji kuchangia damu kwa hiari.

Alisema kitendo hicho pia kinashusha mwamko wa wananchi wanajitokeza kuchangia damu kwa hiari kusaidia wagonjwa wanaohitaji  kwa matarajio wagonjwa watapatiwa huduma hiyo bila malipo.

“Matumizi ya damu ni makubwa kuliko upatikanaji wake, kutokana na  mahitaji kuwa makubwa baadhi ya watumishi wasio waaminifu wamekuwa na tabia ya kuwauzia wagonjwa au ndugu wa wagonjwa damu inayopatikana bure kwenye vituo vyetu vya damu salama” alisemaeza Dkt. Nkya.

 Alisema wale wote wanajihusisha na biashara hiyo waache mara moja kwani inawavunja moyo wale wanaochangia damu kwa hiari bila malipo yoyote na kuwasihi ndugu wanapokutana na watumishi wa aina hiyo kutoa taarifa mara moja kwa uongozi husika.

Dkt. Nkya alisema watakaobainika wakiuza damu hatua kali za nidhamu zichukuliwa dhidi ya watumishi wa aina hiyo pia Mpango wa Taifa wa damu salama umeanza kupita katika hospitali mbalimbali nchini kuhakikisha hakuna watu wanaofanya biashara ya damu.

Mpango wa Taifa wa Damu Salama ambacho kipo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii umekuwa ukikusanya damu kutoka kwa wananchi wanajitolea kusaidia watanzania wenzao wanaohitaji damu kutokana na ajali, uzazi na magonjwa mengine.

 mwisho

No comments:

Post a Comment