Na Peter Mwenda
BOMU la Kutupa kwa mkono ni miongoni mwa silaha 102 zilizosalimishwa kutoka kwa watu waliokuwa wakimiliki isivyo halali kuanzia siku ambayo Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Said Mwema kutangaza miezi mitatu ya kusalimisha silaha hizo.
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Bi. Advela Sinso alisema katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita silaha 5435 zilihakikiwa na 1824 ziliwekewa alama maalum na kuomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano.
Bi. Sinso alisema kati ya silaha zilizosalimishwa ni SMG (26), Rifle (32), Short Gun (24), G.3 (1), SAR (1) na Magobore (16) mkoa wa Rukwa ukiongoza kusalilisha silaha nyingi ikifuatriwa na Mara.
Alisema jeshi la polisi linatoa wito kwa wananchi wanaoendelea kumiliki silaha isivyo halali kutumia kipindi cha miezi miwili iliyobaki kusalimisha silaha hizo na zinazimilikiwa kihalali kuendelea kwenda kuzihakiki katika vituo vya polisi vya wilaya.
Katika hatua nyingine Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani,kimeanza mkakati wa kuondoa ajali za barabarani kushirikisha wadau mbalimbali kwa kufanya ukaguzi kabla ya basi kuondoka stendi na baada ya kufika safari yake.
Kamanda wa Polisi wa Operesheni Maalumu Tanzania, Bw. Saimon Sirro alisema jeshi hilo litaanza kutumia wataalamu Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na askari wa Farasi ili kutafuta chanzo cha ajali za mara kwa mara.
Bw. Sirro alisema ajali za hivi karibuni za basi la Mohamed Trans na Champion zimelifanyua jeshi hilo litafute njia mbadala ya kukomesha ajali hizo.
Katika hatua nyingine Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Bw. Mohamed Mpinga alisema kazi ubadilishaji leseni bado inakwenda kwa kusuasua lakini mpaka sasa madereva 215 wamekamatwa wakiwa na leseni bandia.
Alisema pamoja kuwa jeshi la polisi linaupungufu wa vifaa vya kupambana na wahalifu wa barabarani lakini wananchi wanatakiwa kuonesha ushirikiano wa kutoa taarifa kuhusu dereva ambaye anakwenda mwendo kasi na wasio na leseni kabisa.
Kamanda Mpinga alisema wiki ya Nenda kwa Usalama mwaka huu imesongezwa mbele na sasa itafanyika Oktoba 5 mwaka huu hadi Oktoba 8 ambazo zitafanyika kitaifa mjini Kyela, Mbeya.
mwisho.
No comments:
Post a Comment