TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday, 26 August 2011

'Wakurya 770 wavamia na kupora mashamba Dar, waandishi wanusurika kuchomwa mishale, kukatwa mapanga

Na Peter Mwenda

KUNDI la wananchi wapatao 770, ambao inaaminika ni wazawa wa mkoa wa  Mara "Wakurya" wamevamia mashamba eneo la Pugu Kinyamwezi Kata ya Chanika na Mbondole kata ya Msongola na kujenga nyumba za kuishi na familia zao huku wakilinda makazi hayo na kuwatishia kuwaua wamiliki wa maeneo hayo kutumia pinde, mishale na mapanga.

Sakata la kutishiwa kuuawa kwa mishale na mikuki iliwakuta waandishi nane wa habari kutoka TBC One, Majira, Nipashe, Mwananchi na Wapo Redio walikwenda eneo la Mbondole Kurutini, Kata ya Msongola baada ya kuzingirwa na wakurya hao mara baada ya kuona msafara wa uliongozwa na gari la Polisi wa Kituo cha Stakishari na magari mawili ya Manispaa ya Ilala.

Mkuu wa msafara huo Katibu Tarafa wa Ukonga, Bw. Jeremia Makorere kushirikiana na Mkuu Kituo cha Polisi Stakishari Bw. Jumanne Muliro walilazimika kuwabembeleza watu hao kuweka silaha chini ili waliokuwa wameshika mapanga, mishale na mikuki wakitaka kushambulia msafara huo.

"uuwi!...uuwi!........ tupo tayari kuua mtu, nyie sogeeni muone... kuzaliwa ni bahati kufa ni lazima... alisema mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Bw.Mjinga Hajijui ambaye jina lake halisi ni Msubi aliyekuwa ameshika nondo iliyochongwa na kuwa na ncha kali.


Bw. Msubi na wengine walikimbilia eneo hilo kwa nia ya kuanzisha mashambulizi bila kujali polisi walikuwa wamekaa tayari na silaha zao kuhami msafara huo.

Baada ya Mkuu wa Polisi,Bw. Jeremia Makorere kusema nao Kikurya kushirikiana na Mkuu Kituo cha Polisi Stakishari Bw.Sindalo kuwaomba wasogee eneo la majadiliano watu hao ambao jumla yao walidai wako 370 walisogea eneo hilo ambalo limejengwa za miti na kukandika udongo.


Mbali ya maombi ya Mkuu wa Polisi kutaka watu hao weweke silaha chini wengine waligoma kusogea lakini baadhi waliafanya hivyo na kukubali kuhojiwa na waandishi.

Bw. Msubi alisema kuwa wanataka Serikali iwaruhusu kuchukua eneo hilo kwa sababu hawako tayari kuteseka kuishi nyumba na kupanga wakati eneo hilo limekuwa pori kwa miaka mingi huku likisababisha kuwa kichaka cha vibaka na wahalifu wa kutumia silaha.

Katibu Tarafa wa Ukonga, Bw. Jeremia Makorere alisema eneo hilo ni mali ya Bw. Gina Abbas ambaye alimweka mlinzi wake Bw. Amos Joseph mkazi wa Kurutini ili amlindie lakini watu hao walivamia na kuamua kuvuna mazao na mboga zilizokuwepo kwa madai kuwa ni mali yao.

Katika Kata ya Chanika ambako nako uvamizi kama huo umefanyika, watu 400 wamevamia shamba la Balozi wa zamani Bw. Mwakasyuka lililopo Pugu Kinyamwezi ambako nako wamnejenga nyumba za miti na kuhamia.

Wakizungumza na waandishi wa habari watu hao walidai kuwa wamewahi kumtaka mmiliki alete vielelezo vyake lakini hakufanya hivyo na wao kuamua kuvamia na kufyeka msitu uluiokuwe kufanya makazi.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bw. Leonidas Gama alisema Serikali haiuwezi kuvumilia kuona tabia ya kihuni ya baadhi ya watu kuvamia mashamba ya wananchi kutumia silaha za jadi za pinde,mishale, mikuki na mapanga.

Alisema vikundi hivyo vinavyofanya kazi nyakati za usiku na mchana wakitishia maisha ya wamiliki wa mashamba hayo wanatakiwa kuacha tabia hiyo mara moja kwa sababu sheria itafuata mkondo wake na kujikuta wakitesa familia zao.

Bw. Gama alisema baada ya kupata taarifa za uvamizi huo katika maeneo ya Kata za Chanika, Majohe, Kivule, Msongola na Pugu, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ilikutana Agosti 23 ikiwashirikisha viongozi wa mitaa na kata na kuazimia kupiga marufuku mtu kuingia kwa nguvu katika mashamba ya wananchi waliomilikishwa kihalali kwa nia ya kuvanmia na kuuza.

Alisema kwa mujibu wa tangazo la Serikali na. 231 la 1993 eneo lote la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala lilitangazwa kuwa eneo la Mipango Miji kwa hiyo mwananchi waache kununua ardhi katika mashamba ambayo ni mali halali ya mwananchi aliyehalalishwa na atakayepora eneo au kununua eneo bila kufuata taratibu za kisheria atakuwa amepoteza fedha zake.

mwisho

No comments:

Post a Comment