TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Sunday, 21 August 2011

MWONGOZO WA KATIBA MPYA KWA RAIA HUU HAPA


Stewart Moshi na Servi Roman
MAELEZO
UONGOZI wa Jukwaa la Katiba Tanzania umezindua Mwongozo wa Katiba kwa Raia ili wananchi waweze kujadili na kutoa maoni yatakayowezesha utungwaji wa katiba mpya.
Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw.Deus Kibamba amesema wameandaa Mwongozo wa Katiba ili kuhakikisha mambo yanayopaswa kuzingatiwa katika katiba mpya ya Kidemokrasia yanakuwepo.
Bw.Kibamba amesema mwongozo huo utapatikana bure kwa lugha ya Kiswahili na kwa kila Mwananchi ili kila Mtanzania anayejua kusoma aweze kuielewa na kuchangia mawazo katika uundwaji wa katiba mpya.
Ameelezea kuwa mwongozo uliozinduliwa ni mahsusi katika kuelezea kwa ufundi taratibu na masuala muhimu ya kuzingatia katika mchakato wa kuandika katiba ya kidemokrasia hapa nchini kwetu.
“Mwongozo huo unatoa majibu ya maswali mengi wanayojiuliza Watanzania juu ya mchakato wa Katiba,umeelezea a kwa ufundi na wepesi utaratibu, mchakato wa masuala muhimu ya kuzingatia katika mchakato wa kuandika katiba ya kidemokrasia hapa nchini kwetu”.alisema Bw.Kibamba.
Aidha amesema Mwongozo huo umeangalia historia ya katiba ya sasa ,ikiwemo mabadiliko ya katiba yaliyopita yaliyosukuma upatikanaji wa katiba zote tano za nchi tangu uhuru (Tanganyika na Zanzibar ).
Mwenyekiti huyo amesema mwongozo uliozinduliwa utapatikana kila mkoa bara na visiwani kupitia vituo vya Jukwaa la Katiba Tanzania.

Rais Kikwete afuturu na wakazi wa mkoa wa Lindi aagiza viongozi kutatua tatizo la Maji mjini Lindi

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya wakazi wa mji wa Lindi waliohudhuria futari aliyowaandalia jana jioni mjini Lindi.Rais Kikwete alieleza kusikitishwa kwake na tatizo sugu la maji mji wa lindi na kuwaagiza viongozi wa mkoa huo kutatua tatizo hilo bila kuchelewa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapa zawadi masista wa Kanisa Katoliki mjini Lindi waliohudhuria futari iliyoandaliwa na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mjini Lindi jana jioni (Picha na Freddy Maro).

No comments:

Post a Comment