LIGI ya Taifa ngazi ya Fainali imemalizika juzi kwenye Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga. Timu zilizofanikiwa kupanda daraja la kwanza kwa kuongoza makundi yao ni Polisi Central ya Dar es Salaam, Mlale JKT ya Ruvuma na Mgambo Shooting ya Tanga. Timu zilizopanda kama washindwa bora ni Samaria ya Singida na Small Kids ya Rukwa.
Usajili kwa ajili ya timu za daraja la kwanza utafanyika kuanzia Agosti 15 mwaka huu hadi Septemba 15 mwaka huu. Jumla ya timu 18 zitashiriki ligi inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa Septemba mwaka huu. Taarifa rasmi ya tarehe ya kuanza ligi hiyo itatolewa baadaye.
Timu nyingine za Daraja la Kwanza ni Temeke United ya Temeke, Polisi (Iringa), Burkina Faso (Morogoro), Polisi (Morogoro), Rhino Rangers (Tabora), Polisi (Tabora), 94 KJ (Green Warriors) ya Kinondoni, Tanzania Prisons (Mbeya), Morani (Manyara), Transit Camp (Temeke), Rhino FC (Mbeya), Majimaji (Songea) na AFC (Arusha).
Manyema Rangers ya Ilala, Nyerere FC ya Kilimanjaro na Mwanza United ya Mwanza ndizo zilizoshuka daraja kurudi Ligi ya Taifa.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
VIINGILIO MECHI YA NGAO YA JAMII
Viingilio katika mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) kufungua msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom kati ya mabingwa watetezi Yanga na Makamu Bingwa Simba itakayochezwa Agosti 17 mwaka huu kuanzia saa 2.00 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni kama ifuatavyo;
Viti vya bluu sh. 5,000, viti vya kijani sh. 7,000, viti vya rangi ya chungwa sh. 10,000, VIP C sh. 20,000, VIP B sh. 25,000 na VIP A sh. 50,000. Tiketi zimeanza kuuzwa leo mchana (Agosti 15 mwaka huu) kwenye vituo vyote vya mafuta vya Big Bon jijini Dar es Salaam. Pia zinauzwa katika baadhi ya vituo vya OilCom na TSN.
No comments:
Post a Comment