TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Thursday, 4 August 2011

CUF yavuna wanachama wapya 1,108 kutoka CCM, Chadema

Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimevuna wanachama 1.108 kutoka wilaya ya Kilwa mkoani Lindi ikiwa ni moja ya mikakati yake ya kuhakikisha mkoa huo ni ngome ya chama hicho.

Naibu Katibu Mipango na Bunge wa CUF, Bw. Shaweji Mketo alisema jana Dar es Salaam CUF imebaini mambo makubwa manne ambayo yatafanyiwa kazi kumaliza kero za wananchi wa Kilwa za maji, elimu, afya na miundombinu ya barabara.

Bw. Mketo alisema CUF imejipanga kuchukua jimbo la Igunga, Tabora lililokuwa mbunge wake ambaye alikuwa Mweka Hazina wa zamni wa CCM, Bw. Rostam Aziz aliyejiuzulu kwa kile kinachodaiwa na chama hicho ya kujivua gamba.

No comments:

Post a Comment