TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday, 24 August 2011

Baada ya Luhanjo kumrejesha Jairo kazini, bunge launda Kamati teule kuwajadili

Na Peter Mwenda

BUNGE la Jamhuri ya Muungano limeunda Kamati Teule ya kuchunguza hatua ya Katibu Mkuu Kiongozi, Bw. Philemon Luhanjo kudharau maamuzi ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda na bunge kwa ujumla wake kumsimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. David Jairo kwa madai ya kupenyeza rushwa kwa wabunge.

Aidha wabunge waliopta nafasi ya kuchangia hoja hiyo iliyowasilishwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe waliochangia hoja hiyo walipandwa na mughali wakitaka kujua uwezo wa Luhanjo kudharau bunge na kumwamuru Bw. Jairo kurudi kazini kuanzia leo wakati akijua hayo ni maamuzi halai ya bunge.

"Suala la Jairo lilibuliwa bungeni na lilimgusa sana Waziri Mkuu Peter Pinda,tukaona nini kilichotokea, tunaona kama tumedhalilishwa sana, tunaomba bunge hili tukufu tulijadili"a lisema Bi. Vullu.

Mbunge wa Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini), Zainab Vullu (Viti maalum CCM Pwani), Ole Sendeka (Simanjiro (CCM) walionesha masikitiko makubwa Bw. Luhanjo kujibu ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) Bw. Ludovic Utouh kuwa Bw. Jairo hana kosa.

Hoja hiyo iliungwa mkono na Naibu Spika wa Bunge, Bw.Job Ndugai ambaye alikubali kuundwa kwa kamati hiyo ambayo itatoa ripoti bungeni.

mwisho

No comments:

Post a Comment