TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Friday, 26 August 2011

20 TWIGA STARS KWENDA MAPUTO

TIMU ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twigs Stars) inatarajia kuondoka Agosti 31 mwaka huu kwenda Maputo, Msumbiji kwenye michezo ya All Africa Games itakayofanyika nchini humo kuanzia Septemba 3-18 mwaka huu.
 
Twiga Stars katika msafara wake itakuwa na jumla ya watu 20 ambapo kati yao 16 ni wachezaji na wanne ni viongozi wakiwemo Kocha Mkuu Charles Boniface na msaidizi wake Nasra Mohamed.
 
Mechi ya kwanza ya Twiga Stars itakuwa Septembe 5 mwaka huu dhidi ya Ghana wakati ya pili dhidi ya Afrika Kusini itachezwa Septemba 8 mwaka huu. Twiga Stars itacheza mechi yake ya mwisho katika hatua ya makundi Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe.
 
ALGERIA KUWASILI SEPTEMBA MOSI
Algeria ‘Desert Warriors’ inatarajia kuwasili nchini Septemba Mosi mwaka huu saa 1 jioni kwa ndege ya kukodi ikiwa na msafara wa watu 50 ambapo kati yao 25 ni wachezaji. Timu hiyo itafikia kwenye hoteli ya Golden Tulip.
 
Mechi kati ya Taifa Stars na Algeria itachezwa Septemba 3 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili. Pambano hilo ni la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa Algiers timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
 
Kamishna wa mechi hiyo atakuwa Nicholas Musonye kutoka Kenya wakati waamuzi ambao wote wanatoka Mauritania ni Ali Lemghaifry, Mohamed Hamada, Hassane el Dian a Pene Cheikh Mamadou.
 
LIGI KUU YA VODACOM
Ligi Kuu ya Vodacom kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea tena kesho kwa mechi moja kati ya African Lyon na Toto Africans itakayochezwa Uwanja wa Chamazi ulioko Mbande, Dar es Salaam.
 
Agosti 28 mwaka huu kwenye uwanja huo huo kutakuwa na mechi kati ya JKT Ruvu na Kagera Sugar. Mechi nyingine kwenye Uwanja wa Chamazi itachezwa Agosti 30 mwaka huu kati ya Moro United na Toto Africans.
 
Mechi mbili zitachezwa Agosti 31 mwaka huu ambapo Mtibwa Sugar itakuwa mwenyeji wa Kagaera Sugar katika Uwanja wa Manungu, Morogoro wakati Villa Squad na Polisi Dodoma zitaumana kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
 
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment