MBUNGE wa Jimbo la Monduli ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amewataka wanahabari waamini kuwa Naibu Mhariri wa New Habari 2006 Ltd, marehemu Danny Mwakiteleko amefariki kwa mapenzi ya Mungu.
Akizungumza nyumbani kwa marehemu jana jioni akiwa na mkewe Bibi Regina Lowassa, Waziri Mkuu huyo mstaafu alisema kifo cha Mwakiteleko ni changamoto katika sekta ya habari kufanya kazi hiyo kwa uadilifu kama alivyokuwa akifanya marehemu.
Mwili wa marehemu Danny ulifikishwa nyumbani kwake Tabata Chang'ombe saa 12 jioni na shughuli za kuaga, ibada na maombolezo zitafanyika hapo hapo nyumbani kwake kabla ya kuanza safari ya kwenda Mwakaleli, Tukuyu Mbeya kwa maziko.
No comments:
Post a Comment