TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Saturday, 23 July 2011

Kwa heri Mwakiteleko

Peter Mwenda

NAIBU Mhariri wa New habari (2006) Ltd, Bw. Danny Mwakiteko amefariki dunia alfajiri jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) baada ya kupata ajali mbaya Jumatano iliyopita katika barabara ya Mandela.


Mwakiteleko alilazwa katika kitengo cha watu mahtuti Muhimbili baada ya ajali aliyoipata juzi usiku eneo la Tabata (ToT) na kukimbizwa katika Hospitali ya Amana, Ilala na baadaye Muhimbili.

Katika ajali hiyo gari alilokuwa akiendesha Mwakiteleko liligongwa na lori lenye trela, ambalo lilitoweka bila kujulikana saa nne usiku. Mwakiteleko alikuwa akitokea kazini Sinza ambako alifanya kazi hadi saa tatu usiku.


Mwakiteleko alipelekwa katika Hospitali ya Amana kwa uangalizi hadi saa 12 asubuhi, ambapo madaktari waliamua apelekwe Hospitali ya Tna Stella Aronaifa Muhimbili.

Baada ya uchunguzi Muhimbili, madaktari walisema majeruhi alikuwa ameumia kichwani na kumfanya apoteze fahamu kiasi (semi-conscious) hivyo ikabidi apelekwe katika chumba cha upasuaji ambako madaktari walimhangaikia kuanzia saa sita hadi saa tisa mchana.

Rais Jakaya Kikwete alienda kumuona na kuelezwa kwamba hali yake inaendelea vyema.

No comments:

Post a Comment