TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday, 15 June 2011

TFF yaijia juu Villa Squad

Na Ongetile Osiah, Katibu Mkuu TFF

KAMATI ya Uchaguzi ya TFF, katika kikao chake cha 10 Juni 2011 ilipitia fomu za maelezo ya wagombea uongozi wa Klabu ya Villa na nyaraka za uthibitisho wa sifa za wagombea uongozi.

TFF ilibaini kuwa wagombea Mohamed Kea Mohamed,Ramadhani Soud Iddi, Mohamed Daddy Baucha, Ally Ahamed Mpemba, Said Yusuf Chacha, Idd Mohamed Mbonde na Abdallah D. Majurah hawakidhi  sifa za wagombea uongozi
kama zilivyoainishwa kwenye ibara ya 25 (5) ya Katiba ya Klabu ya Villa.

Kwa kutotimiza masharti na sifa za uongozi kwa mujibu wa Katiba ya Villa, Kamati ya
Uchaguzi ya TFF iliwaondoa katika orodha ya wagombea uongozi kwa nafasi
walizoomba kugombea.

Kamati ya Uchaguzi ya Villa ilitaarifu maamuzi hayo na kuagiza uchaguzi ufanyike kama ulivyopangwa 12 Juni 2011 kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

Nafasi ya Mwenyekiti haina mgombea na itajazwa baadaye kwa mujibu wa Katiba ya Klabu ya Villa Squad Ibara ya 28(c), yaani kwenye uchaguzi mdogo wakati wa mkutano mkuu wa mwaka unaofuata baada ya uchaguzi.

Kamati ya Uchaguzi ya Villa ilitakiwa kwa barua ya TFF yenye kumbukumbu EC/TFF/06/2011/002 ya 10 Juni 2011 kutekeleza maamuzi hayo.

3. KUTOFANYIKA UCHAGUZI WA VILLA
Kutofanyika kwa uchaguzi wa Villa ni ukiukwaji wa Kanuni za uchaguzi za wanachama wa TFF Ibara ya 10 (6) inayokataza kubadili tarehe ya uchaguzi au kufuta uchaguzi ambao umekwisha tangazwa na Kamati ya Uchaguzi bila idhini ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF.

Kutoruhusu Kamati ya Uchaguzi ya TFF ni kukiuka matakwa ya Katiba ya TFF Ibara ya 49(1) inayoipa mamlaka Kamati ya Uchaguzi ya TFF kusimamia chaguzi za wanachama wa TFF.

4.KUBADILI KATIBA BILA IDHINI YA TFF
Kitendo cha kubadili Katiba ya Villa katika mkutano mkuu wa uchaguzi ni kukiuka Katiba ya TFF Ibara ya 12 (1)(b) na (c).

Kubadili vifungu vya Katiba ya Villa na kuweka vipengele vinavokinzana na Katiba ya TFF ni kukiuka Kanuni za Uchaguzi Ibara ya 6(a) na (b) na Katiba ya TFF ya 12 (1) (d) na (e).

Mabadiliko ya Katiba ya Villa yaliyofanywa na tarehe 12 Juni 2011 hayatatambulika na TFF.

5.KUFANYIKA KWA UCHAGUZI WA VILLA ULIOAHIRISHWA KIMAKOSA.
 TFF inaiagiza Kamati ya Uchaguzi ya Villa na uongozi wa Villa kutoendelea na vitendo vya ukiukwaji wa Kanuni za uchaguzi.

TFF inaiagiza Kamati ya Uchaguzi ya Villa na uongozi wa Villa kutekeleza maagizo na maamuzi ya TFF mapema iwezekanavyo kwa kukamilisha mchakato wa uchaguzi kama ilivyoelekezwa na TFF.

TFF inaiagiza Kamati ya Uchaguzi ya Villa na uongozi wa Villa kuhakikisha kuwa inakamilisha mchakato wa uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF na kupata viongozi kabla ya Kikao kijacho cha Kamati ya mashindano ya TFF.

Kikao hicho ambacho kitafanya maamuzi stahiki ya ushiriki wa Klabu ya Villa katika Ligi kuu, endapo Klabu ya Villa haitatekeleza majukmu yake ya kikatiba kwa taratibu zilizowekwa na TFF.

Kamati ya Uchaguzi ya Villa na uongozi wake wanaagizwa kutekeleza maagizo hayo hapo juu ili kuepuka hatua zinazoweza kuchukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za TFF na Katiba ya TFF, CECAFA, CAF na FIFA, endapo hawatatekeleza maamuzi ya TFF.

6.UCHAGUZI WA VIONGOZI WA WANACHAMA WA TFF
Kamati ya Uchaguzi itaendelea na majukumu yake ya kusimamia chaguzi za wanachama wa TFF na inawataka wanachama wote kuzingatia Katiba (zinazoendana na Katiba ya TFF) na
Kanuni za Uchaguzi za wanachama wa TFF na katika michakato ya uchaguzi wa
viongozi wao.

mwisho

No comments:

Post a Comment