TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Wednesday, 11 May 2011

Uzalishaji korosho waongezeka kwa tani 45,000 mwaka 2010/11

Na Peter Mwenda

UZALISHAJI wa zao la korosho nchini umeongeza kutoka tani 75,000 katika msimu wa mwaka 2009/2010 hadi kufikia tani 120,000 katika msimu wa mwaka 2010/2011.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho (TCB) Bw.Hemed Mkali wakati akizungumza na waandishi wa Habari jana, juu ya mafanikio ya zao la korosho nchini.

Alisema kuwa Bodi yake inajivunia kwa kiasi kikubwa kuona wakulima wamezalisha kwa wingi korosho ikilinganishwa na msimu wa mavuno wa mwaka 2009/2010 kwa ongezeko la tani 45,000 kwa msimu huu wa mavuno.

“Hili ni jambo la kujivunia sisi kama Bodi kwani hata mauzo nayo yameongezeka kutoka sh bil. 5 kwa msimu wa mwaka 2009/2010 hadi kufikia sh bil. 22 na hivyo serikali kupata mapato mengi kutokana na mauzo ya zao la korosho” alisema Makali.

Alisema bei ya zao la korosho imefikia kiasi cha sh. 1,000 hadi sh.1,500 kwa kilo na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa mauzo ikilinganishwa na msimu uliopita ambapo bei ya kilo moja ilifikia shilingi 800.


Alisema asilimia zaidi ya 80 ya zao hilo limeuzwa nchini India ambako ndipo hubanguliwa na kiasi kinachobaki huuzwa nchini kwa wazalishaji wa ndani kwa sababu zinazofanya korosho nyingi kuuzwa ghafi, Tanzania haina viwanda vya kutosha ambavyo vingeweza kubangua korosho.

"Serikali inatoa rai kwa wawekezaji wote ambao wamechukua viwanda vya korosho bila kuanza ubanguaji wa korosho kwa lengo la kuongezea thamani bidhaa hiyo kuanza mara moja uzalishaji kwani kuna malighafi ya kutosheleza viwanda vyote nchini ili ziada inayobakia basi iweze kuuzwa nje ya nchi" alisema.

Pia aliwataka wakulima na watu wengine kuunda vikundi ambavyo vitaweza kubangua korosho kuanzia tani moja hadi tano kusaidia kutoa ajira kwa vijana wengi wa kitanzania na kukuza uchumi katika ngazi ya familia.

mwisho

No comments:

Post a Comment