Tweyambe washauriwa kuunda SACCOS
Na Peter Mwenda
KIKUNDI cha kusaidiana cha Tweyambe kimeshauriwa kuanzisha Chama cha Kukopa na Kulipa SACCOS ili kuwanufanisha wanachama wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Ufundi cha Bruni Vocational Training Centre, Bw. Bruno Ndege alisema wanachama wataendelea na moyo wa kukiimarisha chama endapo watapewa nafasi ya kukopa na kuanzisha miradi ya kujikimu kimaisha.
Bw. Ndege alisema kwa kuanzia atatoa komputa moja kwa ajili ya kutunza kumbukumbu za Tweyambe na alitoa sh. 100,000 kwa ajili ya kuanzisha harambee ya kuchangia mfuko huo.
Mwenyekiti wa kikundi cha Tweyambe, Bw. Revocatus Karugaba alisema wamekubali ushauri huo na kuahidi kuwa fedha zilizochangwa wanachama zimefikia sh. mil. 2.1 na zimehifadhiwa benki.
Wamejiwekea malengo ya kuahidi kufungua Saccos hiyo mapema iwezekanavyo ili wanachama na waengine wakope ili kufungua miradi.
Alisema chama hicho kinahitaji vifaa vya ofisi kama komputa, mashine ya kudurufu, na vifaa vingine vinavyofikia sh. mil. 5.
mwisho
No comments:
Post a Comment