Keko Mwanga Development Foundation (KEMWADEFO)
S.L.P 50167
Dar es Salaam
23.12.2010
Taasisi ya Keko Mwanga Development Foundation inakialika chombo chako cha habari kuhudhuria uzinduzi wa ugawaji mipira kwa timu 10 za Keko Mwanga.
Timu hizo zitakazokuwa na wachezaji wa chini ya miaka 20 ndizo zitakazoshiriki mashindano ya kumuenzi mwaasisi wa soka Keko Mwanga, Miraji Salum (Kizoka).
Halfa ya kugawa mipira hiyo yenye thamani ya sh. 400,000 zitafanyika Jumapili 26/12/2010 (Boxing Day) katika ukumbi wa Baa ya Matimila, Keko Mwanga saa 4.00 asubuhi.
Kutokana mchango wa chombo chako katika kutangaza na kuelimisha jamii kupitia michezo, taasisi hii inaomba ushirikiano wako kuungana nasi kufufua michezo ambayo ilikuwepo eneo la Keko Mwanga lakini baadaye ilikufa baada ya uwanja uliokuwa unatumika kwa michezo (Sulurele) kujengwa shule ya msingi.
Timu kumi zitakazokabidhiwa mipira kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Kizoka Cup ni Eleven Fighters FC, Wasouth FC, Host Boys FC, Tumetumwa Ushindi FC, na Only Work FC kutoka kundi A.
Kundi B ni timu za Pasindefu FC, Corner Boys FC, Mpira Kipaji FC, Rangers FC na First Wazawa FC kutoka Kundi B ambazo zitaanza mashindano hayo Januari 15 katika uwanja wa G.T.A uliopo M.T Depot, Darajani karibu na Wizara ya Maliasili na Utalii.
Katibu wa KEMWADEFO
Peter Mwenda
0752,0786,0772, 0715 222677
e-mail mwendapeter5@yahoo.com
e-mail petermwenda0@gmail.com
website;www.mwendanews.blogspot.com
ACHA MADAWA YA KULEVYA, UHALIFU,NGONO ZEMBE NA ENDELEZA MICHEZO.
No comments:
Post a Comment