TANGAZO ISERESPORTS COLLECTION

TANGAZO SHIWATA

Tuesday 14 August 2018

KEKO FURNITURE NA GOMS UNITED SASA KUKUTANA KATIKA MASUMBWI SEPTEMBA 15 TAIFA



FRED SAYUNI
Na Mwandishi Wetu 

Haidari Mchanjo
Katika ali iliyo ya kawaida kwa mashabiki wa michezo baada ya kucheza mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kama Ndondo Cup sasa timu za Goms United na Keko Furniture kukutana katika masumbwi ambapo Goms united inawakilishwa na bondia Haidari Mchanjo na KekoFurniture anatoka Fred Sayuni 

Mabondia hawo wamesaini mkataba na watazipiga siku ya Septemba 15  katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa Indoor Stadium akizungumza baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Sayuni amesema kama kawaida yake anawambia mashabiki wake wote wa Keko kuwa yupo vizuri na anajiandaa kushinda ushindi wa kishindo 

ambapo kwa sasa anafanya mazoezi ya kutosha ili awafurahishe mashabiki wake ili waweze kumpa sapoti ya mana awze kuendelea na kipaji chake mbele zaidi 

Nae Mchanjo amejinasibu kwa kusema Sayuni ni bondia wa zamani hivyo nitamfanyia kitu mbaya kama nilivyo mfanyia Cosmas Cheka mana nilimpiga kama begi nae afanye mazoezi ili nisije nikamuaibisha mbele ya mashabiki wake

nawaomba mashabiki wangu wote wale wa goms pamoja na viunga vyake waje kuangalia kazi nitakayofanya siku hiyo

Akizungumzia mpambano mratibu wa mapambano ya ngumi Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali ya ngumi wakati Abdallah Pazi 'Dula Mbabe' atazipiga na Geoger Dimoso na Vicent Mbilinyi atavaana na Saidi Mpoma 'Kidedea' wakati Mohamedi Kashinde atakumbana na Sadiki Momba na Imani Daudi ataoneshana umwamba na Paul Kamata 

Na mpambano mwingine utawakutanisha Faraji Sayuni na Issa Nampepeche Ramadhani Shauri atakumbana na Said Amani wakati Mwinyi Mzengela atakumbana na Kassimu Rajabu 'Boxer Mnyama' Saidi Zungu na Tonny Rashidi

mapambano hayo yameandaliwa na  kampuni ya ngumi za kulipwa ya Super D Boxing Promotion inayoendelea kuinuwa vipaji vya mabondia mbalimbali nchini ili kujikuzia kipato na kujiweka nafasi nzuri kwa mabondiakucheza kula wakati

No comments:

Post a Comment